Home Mchanganyiko WANAWAKE TUGHE PWANI WATOA MSAADA KWA WANANCHI WALIOKUMBWA NA MAFURIKO RUFIJI

WANAWAKE TUGHE PWANI WATOA MSAADA KWA WANANCHI WALIOKUMBWA NA MAFURIKO RUFIJI

0

Mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi wanawake  wa serikali na afya (TUGHE) Mkoa wa Pwani Catherine Katele kulia akimkabidhi msaada wa magunia ya mahindi Katibu Tawala wa Wilaya ya Rufiji Maria Katemana kwa ajili ya kuwapatia wananchi waliopata maafa ya mafuriko kutoka na mvua zilizonyesha hivi karibuni.(PICHA NA VICTOR MASANGU)

Baadhi ya wanawake wa Chama cha Tughe Mkoa wa Pwani wakiwa wanatoa msaada wa mahindi kwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Rufiji akiwa ameongozana na viongozi mbali mbali wa serikali kwa ajili ya kuwapatia wananchi ambao mazao yao yamesombwa na maji na wengine nyumba zao kuzingirwa kutoka na mafuriko yaliyotokea.(PICHA NA VICTOR MASANGU)

Wanawake wa chama cha Tughe Mkoa wa Pwani wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbali mbali wa serikali wakiongozwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Rufiji mara baada ya halfa fupi ya kukabidhi magunia ya mahindi lengo ikiwa ni kuwapatia wananchi ambao wamekumbwa na maafa ya mafuriko na kusababisha mazao yao kusombwa na maji.(PICHA NA VICTOR MASANGU)

Katibu Tawala wa Wilaya ya Rufiji Maria Katemana akizungumza jambo na baadhi ya viongozi wa wanawake wa Tughe Mkoa wa Pwani walipofika ofisini kwake kwa ajili ya kujitambulisha na kutoa msaada wa magunia ya mahindi pamoja na vyakula mbali mbali wa wananchi ambao wanamahitaji kutokana na kupata mafuriko.(PICHA NA VICTOR MASANGU.)

Mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi wanawake wa serikali na afya (TUGHE) Mkoa wa Pwani Catheline Katele akifafanua jambo kwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Rufiji hayupo pichani kuhusiana na ujio wao wa kufanya ziara maalumu yenye lengo la kutoa msaada wa vyakula mbali mbali ikiwemo magunia ya mahindi kwa ajili ya wahanga wa mafuriko.(PICHA NA VICTOR MASANGU)

Katibu Tawala wa Wilaya ya Rufiji Maria Katemana akiwa na wanawake wa Tughe Mkoa wa Pwani wakiwa wanatembea kwa furaha mara baada ya kumalika kwa sherehe ya kutoa msaada wa vyakula mbali mbali ikiwemo magunia ya mahindi ambayo yametolewa kwa ajili ya kuwasaidia wananchi waliokumbwa na mafuriko(PICHA NA VICTOR MASANGU)

Baadhi ya viongozi wa Tughe Mkoa wa Pwani wakiwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Rufiji wa kati kati wakipiga makofi ikiwa ni ishara ya kufurahi mara baada ya kumaliza kutoa msaada wa magunia ya mahinda kwa waananchi waliokubwa na maafa ya mafuriko.(PICHA NA VICTOR MASANGU)

Baadhi ya wanawake wa Tughe Mkoa wa Pwani wakiwa wanaimba nyimbo maalumu mara baada ya kuwasili katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Rufiji kwa ajili ya halfa ya kukabidhi mahitaji mbali mbali kwa wananchi ambao walipatwa na mafuriko na mazao yao kusombwa na maji na wengine nyumba zao kuzingirwa na maji.(PICHA NA VICTOR MASANGU)

*********************

VICTOR MASANGU, RUFIJI

Baadhi ya wananchi Wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani wamekosa makazi ya kuishi kutokana na nyumba zao pamoja na maduka  kuzingirwa na maji  ikiwemo wengine kukumbwa na changamoto ya mazao yao mbali mbali  zaidi ya hekta 4000 kusombwa na maji kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha na kusababisha maafa  hayo ambayo yamepelekea wananchi kuishi katika mazingira magumu  hivyo kupelekea kuishi katika mazingira magumu.

Hayo yalibainishwa  na wananchi hao wakati wa ziara ambayo imefanywa na Wanawake wa  chama cha wafanyakazi wa serikali na afya (TUGHE) Mkoa wa Pwani  yenye lengo la kutembelea  baadhi ya maeneo ambayo yamekumbwa na maafa ya mafuriko  kwa ajili ya  kutoa msaada wa vyakula kwa walengwa.

Wananchi hao wakizungumza kwa nyakati tofauti akiwemo Shamte Ally na Said Salumu walisema walidai kwamba  mvua  ambazo zinaendelea kunyesha kwa kipindi hiki zimewaletea hasara kubwa ya mazao yao, mifugo, pamoja na makazi kuzingirwa na na maji hivyo wameimba serikali ya awamu ya tano kuwasaidia  msaada wa kupata chakula  pamoja na sehemu  kwa ajili ya  kuishi.

Aidha waliongeza kuwa kwa sasa kutokana na kuwepo kwa hali hiyo baadhi ya bidhaa ya vyakula katika maeneo mengine zimepanda bei hivyo wengine kutokana na kipato chao kuwa cha chini wanashindwa kumudu gharama kwa ajili ya kununua vyakula hivyo wameomba wadau mbali mbali kwa kushirikiana na serikali kuliangalia suala hilo kwa jicho  la tatu katika kuwasaidia kuondokana na hali hiyo.

“Kwa kweli ndugu waandishi kwanza tunashukuru sana hawa wakinamama wa Tughe Mkoa wa Pwani kwa kuweza kuja mpaka uku katika maeneo ya Rufiji, kwani kwa sasa tupo katika hali ngumu sana kutokana na mazao mbali mbali ya chakula ambayo ndio tulikuwa tunayategemea sisi pamoja na watoto wetu yote wamesombwa na maji, lakini pia tunashukuru kupatiwa msaada huu lakini bado tunahitaji zaidi ili tuweze kujikimu,” walisema wananchi hao.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Wilaya ya Rufiji Maria Katemana alikiri  kuwepo kwa maafa hayo na kubainishwa kwamba  hadi sasa zaidi ya hekta 4000 za mazao ya aina mbali mbali ikiwemo mahindi mpunga,  yamesombwa na maji ambapo  pia kuna baadhi ya shule nne  za msingi zimefungwa kwa muda kutokana na  kuwepo kwa hali hiyo ya mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

“Kwanza kabisa napenda kutoa shukrani zangu kwa niaba ya serikali ya Wilaya ya Rufiji kwa msaada huu wa chakula cha mahindi ambao umetolewa na Wanawake wa Tughe Mkoa wa Pwani kwa lengo la kuwasaidia baaadhi ya wananachi amabao wamekumbwa na mafuriko hayo ambayo kwa kweli yamesabisha hekta  zaidi ya 4000 za mazao kusombwa na maji na kuna maeneo mengine ya shule bado maji yapo, hivyo tunaendelea kujitahidi kwa hali na mali ili wanafunzi waweze kuendelea na masomo yao, alisema Maria.

Kufuatia kutokea kwa  maafa hayo ya mafuriko Wanawake kutoka chama cha wafanyakazi wa serikali na afya (TUGHE) Mkoa wa Pwani  wameguswa na tukio hilo na kuamua kwenda kutoa msaada wa vyakula mbali mbali ikiwemo mahindi kwa wananchi ambao wamekubwa na maafa ya  mafuriko hayo kwa lengo la kuwasaidia kuweza kupata chakula ikiwemo kupata mbegu kwa ajili ya kupanda tena kutokana na mazao yao yaliyosombwa na maji.

Mwenyekiti wa chama cha wafanyakazi wanawake  wa serikali na afya (TUGHE) Mkoa wa Pwani Catherine Katele alisema kwamba waliamua kwenda kutembelea baadhi ya maeneo ambayo yamekumbwa na mafuriko  na kutoa msaada wa vyakula kama mahindi ambayo yatawasaidia wananchi kuweza kupata chakula na mengine kuyatumia kwa ajili ya  kupanda mazao mengine ambayo yamekwenda na maji.

“Sisi kama wanawake wa tughe Katika Mkoa wa Pwani kwa kweli tumegiswa sana na jambo hili la wenzetu wa Rufiji kupata maafa ya mafurikio, hivyo ktukaona ni vema tufunge safari ya kuja mpaka huku na kweli tumjionea jinsi ya nyumba mbali mbali ambanzo zimezingirwa na maji na mazao ambayo yamesombwa na maji kwa hiyo kwa hiki kidogo tulichokitoa cha msaada wa mahindi kitaweza kuwasaidia kwa namna moja hama nyingine na pia tutazidi kuendelea kutoa misaada mbali mbali kwa watu wenye mahitaji, “alisema Katele.

Wilaya ya Rufiji iliyopo Mkoa wa Pwani ambayo ina jumla ya kata zipatazo 13 imekuwa ikikabiliwa na changamoto ya maafa ya mafuriko hasa katika kipindi cha mvua zinaponyesha kutokana na baaadhi ya maeneo kuwepo pembezoni mwa mto Rufiji hivyo kupelekea baadhi ya mazao kusombwa na maji na nyumba nyingine kuzingirwa na maji na kusababisha wananchi kuishi katika mazingira magu