Home Mchanganyiko VANDENBROECK NA VITALIS MAYANGA WATWAA TUZO YA MWEZI WA PILI LIGI KUU

VANDENBROECK NA VITALIS MAYANGA WATWAA TUZO YA MWEZI WA PILI LIGI KUU

0

Mshambuliaji wa Ndanda SC ya Mtwara, Vitalis Mayanga amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Februari wa Ligi Kuu Tanzania akiwashinda Reliants Lusajo na Bigirimana Blaise wa Namungo FC.

Naye Sven Vandenbroeck wa Simba ameibuka kuwa kocha bora wa mwezi huo akiwashinda Hatimana Thiery wa Namungo na Abdul Mingange wa Ndanda.