Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. Mussa Zungu akisalimiana na
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Hemedi Suleiman wakati alipowasili kisiwani Pemba kwa ajili ya ziara
ya siku moja kutembelea eneo la kwa Mgogo lililoharibika na athari za mabadiliko ya tabia nchi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. Mussa Zungu akielezea jambo
wakati wa ziara ya kutembelea kijiji cha Kwamgogo kilichoko kisiwani Pemba ambapo alienda kujionea
athari za kimazingira katika kijiji hiko ambazo zimesababishwa na mabadiliko ya tabianchi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. Mussa Zungu akiongea na
Wananchi wa kijiji cha Kwamgogo mara baada ya kumaliza ziara ya kutembelea kijiji hiko kilichoathiriwa
na mabadiliko ya tabianchi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. Mussa Zungu akiwa katika picha
ya pamoja na viongozi wa serikali wa Mkoa wa kusini Pemba pamoja na Wananchi na watoto waliohudhuria katika mkutano wake na Wananchi wa kijiji cha Kwamgogo alikofanya ziara kujionea athari za kimazingira zilizosababibishwa na mabadiliko ya tabia Nchi.
******************************
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mh. Mussa Zungu amaeahidi kupeleka Wataalamu wa mazingira kwa ajiili ya kufanya tathmini katika eneo la Kwamgogo lililopo Kisiwani Pemba ambalo limeathirika na mabadiliko ya tabianchi. Amesema hayo kisiwani Pemba
alipotembelea eneo hilo kujionea athari za kimazingira zilizosababishwa na mabadiliko ya tabinchi.
Ameongeza kuwa lazima jitihada za haraka zichukuliwe katika eneno hilo ili kuweza kuepusha kisiwa cha
Pemba kisiharibiwe na mabadiliko ya tabianchi. “ tutaleta Watu wafanye tahtmini ni kitu gani tufanye ili
kuzui haya maji kuja tena au kuyazuia yarudi huko yalikotoka na kuweza kunusuru eneno hili”alisema
Waziri Zungu.
Kijiji cha Kwamgogo kimeathirika na mabadiliko ya tabianchi kwa kusababisha maji kujaa na kuharibu mazingira ikiwemo kusababisha Wananchi kukosa njia ya kupita wakati wanaenda sokoni au kwenye shughuli zao za kila siku hivyo kusababisha Wananchi kuvuka kwa kuogelea kwenda ng’ambo ya pili kwenye huduma muhimu za kijamii.
Amewashukuru pia Wananchi wa Mkoa huo na Uongozi wa Mkoa kwa kuweza kuchukua hatua kwa kupanda mikoko na ili kuweza kupunguza athari hizo za kimazingira katika kijiji hiko cha Kwamgogo.
“Namshukuru saana Mkuu wa Mkoa pamoja na Wananchi wa eneo hili kwa jitihada mlizofanya kulinda mazingira katika eneo hili” alisema Zungu Ziara hiyo ya Mheshimiwa Zungu ni maagizo aliyopewa na Makamu wa pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi baada ya kumtembelea Ofisini kwake kujitambulisha baada ya kuchaguliwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira.