Home Mchanganyiko Ofisi ya mbunge yafungua dawati la ujasirimali Arumeru Mashariki

Ofisi ya mbunge yafungua dawati la ujasirimali Arumeru Mashariki

0

***********************

Na Queen Alex Meru

Ofisi ya mbunge wa Jimbo la Arumeru mashariki imefungua dawati la Vijana la ujasiriamali  ndani ya ofisi hiyo ili kuweza kuwapatia Vijana elimu ya kilimo,ujasiriamali na ufugaji ambayo itawawezesha kujiajiri   wenyewe na hatimae waweze kuondokana na tatizo la ajira.

Hayo yameelezwa na katibu  msaidizi kuwa mbunge wa Jimbo la Arumeru mashariki Hungura mbwana wakati akizungumza na wananchi wa kata ya mbuguni iliyopo wilayani Arumeru Mara baada ya mbunge wa Jimbo Hilo kufanya ziara ya kutembelea wananchi wa kata hiyo.

Hungura Amesema kuwa ofisi ya mbunge huyo iliamua kufungua dawati Hilo  Mara baada ya kubaini uwepo wa changamoto za Vijana kutokuwa na elimu ya  maisha ya mtaani ya kujiajiri

Katibu Hungura  Amedai kuwa dawati  Hilo ambalo  linatoa elimu  bure kwa makundi yote ikiwemo Vijana  akina mama na akina baba itasaidia kujiajiri wenyewe kufuatia ajira kuwa ngumu serikalini.

Kwa upande wake kiongozi wa dawati Hilo bw Creino isangya Amesema kuwa uwepo wa dawati Hilo unawezesha kuwaunganisha vijana pamoja  kwa kutumia  kauli mbiu  ya kutumia ulicho nacho kupata ambacho hauna.

Amefafanua kuwa kupitia makundi ya   vijana ambayo yataundwa na watu kumi Mara baada ya kupata mradi wautakao ofisi itawasaidia kuwatengenezea andiko la mradi,katiba,usimamizi ktk utekelezaji pamoja na kupatiwa elimu ya mradi husika.

Awali mbunge wa Jimbo Hilo John Danielson palangyo amesema Nia ya serikali ya awamu ya tano Ni kuhakikisha inatatua changamoto zinazowakabili wananchi hivyo ataendelea kushiriki kikamilifu katika kutatua changamoto zinazowakabili ili abadilishe maisha ya watanzania.