Home Mchanganyiko Wafanyakazi wa Vodacom Kanda ya Kaskazini watembelea kinamama waliojifungua Hospitali ya Tengeru...

Wafanyakazi wa Vodacom Kanda ya Kaskazini watembelea kinamama waliojifungua Hospitali ya Tengeru mkoani Arusha na kuwafariji ikiwa ni sehemu ya kuelekea siku ya Wanawake Duniani

0

Mkuu wa mauzo wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania PLC kanda ya kaskazini,  Brigita Stephen akikabidhi vifaa mbalimbali kwa niaba ya wafanyakazi wa Vodacom kanda hiyo kwa wakinamama waliojifungua na wanaotarajia kujifungua kwenye Hospitali ya Tengeru iliyopo Halmashauri ya Meru jijini Arusha leo, Ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani, ambapo kauli mbiu yao ni “uwajibikaji wa uongozi katika kujenga kizazi cha usawa wa Jinsia” 

Meneja wa VBU, Scola Lyakurwa akizungumza na Madaktari na Wauguzi wa Hospitali ya Tengeru mara baada ya kutoa vifaa mbali mbali ikiwa sehemu ya kuwafariji wakinamama waliojifungua na wanaotarajia kujifungua kuelekea siku ya wanawake Duniani.