Home Siasa MLOZI ATOA PONGEZI KWA JPM UTEUZI WANAWAKE

MLOZI ATOA PONGEZI KWA JPM UTEUZI WANAWAKE

0

Katibu wa Jumuia ya Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT-Taifa) Queen Mlozi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuelekea siku ya maadhimisho ya wanawake Dunia ambayo hufanyika kitaifa Machi 8 kila mwaka na yanatarajia kufanyika kitaifa mkoani Simiyu.

……………………………………………………………………………………………

Na.Alex Sonna,Dodoma

 Katibu wa Jumuia ya Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT-Taifa) Queen Mlozi amemuomba Rais,Dk.John Magufuli kuendelea kuwapa Wanawake nafasi za uongozi kutokana na waliopo kufanya vizuri kwenye awamu yake ya tano.

Bi.Mlozi ametoa ombi hilo leo jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea siku ya maadhimisho ya  wanawake Dunia ambayo hufanyika kitaifa Machi 8 kila mwaka na yanatarajia kufanyika kitaifa mkoani Simiyu.

Aidha Bi.Mlozi amesema kuwa  katika Awamu ya Tano nchi imeweka historia ya pekee kwa kumteua  Makamu wa Rais, mwanamke Samia Suluhu Hassan, Naibu Spika ,Dk.Tulia Ackson, mawaziri, manaibu na ngazi nyingine mbalimbali.

Bi.Mlozi amesisitiza kuwa wanawake ambao walipewa nafasi mbalimbali za uongozi hawajamuangusja Rais kwenye kazi wamekuwa wakifanya vizuri  katika utekelezaji wa majukumu yao.

“Kiukweli kabisa tunampongeza Rais wetu Dkt.Magufuli kwa kuandika historia ya kuwateuwa wanawake katika uongozi mbalimbali hivyo tunamuomba endelee kuwateua kwenye nafasi nyingi ili hatimaye tuweze kufikia katika asilimia 50% kwa 50%”amesema Mlozi 

Hata hivyo amesema kuwa wanawake wanatakiwa kujiamini,wenye ujasiri,wenyer busara na kuweza kujiona kuwa wanathaminiwa na kuacha kuwa wanyonge kwani kinachotakiwa hapo ni usawa kati ya mwanamke na mwanaume.

Aidha amesema kuwa kipindi hiki nchi inaelekea kwenye uchaguzi hivyo wananchi wanatakiwa kuwa makini na kuwachagua viongozi wenye ueledi na uwezo wa kutafsiri Ilani ya CCM.

Bi.Mlozi amewataka wanawake kumpigia  kura za kishindo rais na viongozi wengine watakaojitojeza kuchukua fomu kwa ajili ya kugombea nafasi mbalimbali hususani wanawake ili waweze kushinda katika nafasi hizo.

“Wanawake ni kioo Cha Jamii na kielelezo hata katika familia au kwenye maendeleo hivyo  lazima wawe kifua mbele Kupambana na udhalimu, ukatili na unyanyasaji wa kijinsia wa aina yeyote ile,”amesisitiza Bi.Mlozi