Home Michezo SIMBA SC YAICHAPA 3-2 AZAM FC ,YATUMA SALAMU KWA YANGA MACHI 8

SIMBA SC YAICHAPA 3-2 AZAM FC ,YATUMA SALAMU KWA YANGA MACHI 8

0

…………………………………………………………………………………….

Simba imeendeleza ubabe kwa Azam Fc baada ya kuwachapa mabao 3-2 mchezo wa Ligi Kuu Tanzania bara uliomalizika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mchezo ulikuwa mkali kwa kila timu na kuwa na mvuto wa kutazama Azam FC walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 4 kupitia kwa kiungo wao Mzimbabwe Never Tegere.

Hata hivyo Simba walisawazisha kupitia Erasto Nyoni dakika ya 8 na bao la pili likifungwa na Deo Kanda dakika ya 14 hadi mapumziko Simba walienda mapumziko wakiwa mbele ya mabao hayo mawili.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko na katika dakika ya 49 Azam Fc walisawazisha bao kupitia Suleiman Idd Nando akimalizia pasi ya Shaban Chilunda.

Akitokea benchi mshambuliaji na mvumania nyavu Meddie Kagere alifunga bao la tatu na la 15 msimu huu wa Ligi akimalizia pasi ya Shomari Kapombe dakika ya 71 na kuiwezesha Simba kuondoka na Pointi tatu Muhimu.

Obrey Chirwa alitungua Aish Manula dakika ya 83 lakini mwamuzi alitafsri kuwa ameoteana kwa matokeo hayo Simba imefikisha Pointi 68 na kuendelea kujiweka kwenye nafasi ya kutetea ubingwa huku Azam Fc akibaki nafasi ya pili kwa Pointi 48.

Kwa ushindi huo Simba inaingia msituni kwa mawindo dhidi ya watani wao Yanga kwa mchezo utakaopigwa uwanja wa Taifa siku ya Jumapili Machi 8.

Azam FC inashambulia kwa kushtukiza huku Simba ikiwa kwenye mpango wa kutengeneza nafasi
Dakika moja inaongezwa
Mchezaji wa Azam FC anakuwa wa kwanza kuonyeshwa kadi ya njano Uwanja wa Taifa

Dakika ya 14 Kanda anafunga Goaaal la pili Dakika ya 8 Nyoni anafunga bao kwa kichwa  Dakika ya 4 Nevere Tegere anamtungua Aish Manula kwa guu la kulia

AZAM FC leo imeikaribisha Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara Uwanja wa Taifa.

Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Taifa Azam FC ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 mfungaji akiwa ni Meddie Kagere hivyo leo ni mchezo wa kisasi.