Home Mchanganyiko TANROADS YATOA TAARIFA KUHUSU KUVUNJIKA KWA DARAJA LA KIYEGEYA (MAGUBIKE)

TANROADS YATOA TAARIFA KUHUSU KUVUNJIKA KWA DARAJA LA KIYEGEYA (MAGUBIKE)

0

************************

Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) inautarifu Umma kuwa sehemu ya barabara eneo la Kiyegeya (Magubike) katika Wilaya ya Kilosa kwenye Barabara Kuu ya Morogoro – Dodoma imekatika na hakuna mawasiliano kati ya Mikoa hiyo kufuatia mvua kubwa inayoendelea kunyesha.

 

Kufuatia hali hiyo, TANROADS inawaomba watumiaji wa barabara ya Morogoro – Dodoma kutumia viunganisho mbadala ikiwemo barabara ya Morogoro – Iringa – Dodoma na mikoa mingine ya kanda ya kati katika kipindi hiki ambacho matengenezo katika eneo hilo yakiendelea.

 

TANROADS inasikitika kwa usumbufu uliojitokeza wakati tunaendelea na huhudi za kurudisha mawasiliano katika barabara hiyo.