Home Mchanganyiko TAASISI YA EANNASO YAHAMASISHA UPATIKANAJI WA TAARIFA ZA AFYA

TAASISI YA EANNASO YAHAMASISHA UPATIKANAJI WA TAARIFA ZA AFYA

0
Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Eannaso,Olive Mumba akizungumza katika kongamano lililofanyika jijini Arusha

 

Programu Meneja wa Eannaso,Onesmus Mlewa akizungumza namna kanzi data ya taarifa walizokusanya zinavyowasaidia watumiaji ulimwenguni.

 

Wadau mbalimbali walioshiriki katika kongamano hilo wakifatilia mada kwa umakini.

Mwandishi WetuArusha.
Taasisi isiyo ya kiserikali inayojihusisha na sekta ya Afya
katika nchi za Mashariki mwa Afrika(EANNASO) imesema taarifa zinazohusu
upatikanaji wa huduma za afya zimekua hazipatikani kikamilifu na kusababisha
hofu kwa watu wenye kuzihitaji.
Mkurugenzi wa taasisi hiyo,Olive Mumba amesema hayo wakati
akizungumza katika kongamano la wadau kutoka Kenya na Tanzania juu ya
upatikanaji wa taarifa muhimu wa namna wananchi wanaoishi katika mipaka ya nchi
wanachama wa EAC wanaweza kupata huduma hizo.
Amesema nchi sita za EAC zina idadi ya wananchi
wasiopungua milioni 177 ambao wanahitaji huduma bora za afya lakini wakati
mwingine wamekua wakilazimika kwenda maeneo ya mbali wakati huduma hizo
zinapatikana karibu.
“Magonjwa hayana mipaka ya nchi na eneo la EAC lipo
kwenye hatari ya magonjwa ya ina mbalimbali yakiwemo ya milipuko, pia tunao
watu takribani milioni sita wanaoishi na maambukizi ya VVU ni muhimu wananchi
kuwa na taarifa za uhakika sehemu ya kupata huduma,”amesema Mumba
Meneja Programu wa taasisi hiyo,Onesmus Mlewa amesema
wamewaleta pamoja wadau wanaoishi katika mpaka wa Kenya na Tanzania wa Namanga
ili kuwashirikisha mpango huo na wao kutoa maoni ya namna wangependa kupata
taarifa za afya.
“Unakuta kuna mwananchi
anayeishi na Virusi vya Ukimwi katika nchi ya Kenya anatumia dawa za
kufubaza makali ugonjwa anataka kusafiri kuja Tanzania ni muhimu awe na taarifa
atakapofika Dodoma au Morogoro akihitaji dawa atazipata wapi,hizi ni taarifa
muhimu kila mtu kuwa nazo,”amesema Mlewa
Amesema wananchi wamekua wakifuata huduma za afya sehemu
za mbali wakati zinapatikana maeneo ya jirani jambo hili linasababishwa na
kutokua na taarifa sahihi na haitoshi kwa serikali kusema dawa na wataalamu
wapo bali taarifa ziwekwe katika njia rahisi ya kila mtu kuzipata.
Naye Mratibu wa mradi huo,Nginael Mariki amesema utekelezaji
wa mradi huo utaanzia katika mpaka wa Namanga kisha katika mipaka mingine kwani
maeneo ya mipakani kumekua na mwingilino wa kibiashara na kijamii ambao unaweza
kueneza magonjwa ya milipuko.