Home Michezo MBUNGE WA JIMBO LA WAWI CUF VISIWANI PEMBA AJIUNGA NA CCM

MBUNGE WA JIMBO LA WAWI CUF VISIWANI PEMBA AJIUNGA NA CCM

0

………………………………………………………………………………………………………

Akiwa katika ziara ya kukagua na kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015 – 2020 Wilaya ya Chakechake Mkoa wa Kusini Pemba Zanzibar Ndugu Humphrey Polepole Katibu Mwenezi wa CCM Taifa amepokea maombi ya Mbunge wa Jimbo la Wawi kwa tiketi ya CUF kuomba kujiunga na CCM.

Hatua hiyo imekuja baada ya Ndugu Ahmed Juma Ngwali kuusimamisha msafara wa Ndugu Polepole, kuomba kujiunga na CCM na kutangaza kujivua nafasi zake zote ndani ya Chama cha CUF.