Home Michezo SIMBA YAICHAPA 2-0 KMC,MIQUISSONE AITUMIA SALAMU YANGA

SIMBA YAICHAPA 2-0 KMC,MIQUISSONE AITUMIA SALAMU YANGA

0

Simba wameendelea kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kutetea ubingwa wao wa Ligi Kuu Tanzania bara baada ya kuichapa 2-0 KMC Mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mchezo wa Simba dhidi ya KMC ulionekana kuwa mgumu kwa pande zote mbili kutokana na ubora wa timu hizo hadi mapumziko hakuna aliyekuwa kamtambia mwenzake.

Shujaa wa Simba ni winga wa kimataifa toka Msumbiji Luis Miquissone aliyewapa raha mashabiki wa Simba kwa kufunga mabao 2 peke yake dakika ya 70 na 72.

Simba itajitupa tena uwanjani Machi 3 kucheza na Azam Fc katika uwanja wa Taifa kabla ya kuwavaa watani zao Yanga Machi 8.