Home Michezo MASHINDANO YA MAKISATU  KUFANYIKA MACHI 16-20 MWAKA HUU UWANJA WA JAMHURI DODOMA

MASHINDANO YA MAKISATU  KUFANYIKA MACHI 16-20 MWAKA HUU UWANJA WA JAMHURI DODOMA

0

Mkurugenzi idara ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu kutoka Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,Prof.Maulilio Kipanyula,akizungumza na waandishi wa habari kwenye kikao kazi kinachohusu mashindano ya Kitaifa ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) yanayotarajia kuanza Marchi 16 hadi 20 mwaka huu uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini  ,Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Sylvia Lupembe,akielezea umuhimu wa mashindano hayo kwa waandishi wa habari ambayo yanayotarajia kuanza Marchi 16 hadi 20 mwaka huu uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Sehemu ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakimsikiliza Mkurugenzi idara ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu kutoka Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,Prof.Maulilio Kipanyula,wakati wa kikao kazi kinachohusu mashindano ya Kitaifa ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) yanayotarajia kuanza Marchi 16 hadi 20 mwaka huu uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Mwandishi wa habari toka TBC Aneth Andrew,akiuliza swali kuhusu jinsi ya wabunifu wanavyoshiriki na kuibuka washindi wanasaidiwaje kwa Mkurugenzi idara ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu kutoka Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,Prof.Maulilio Kipanyula

……………………………………………………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Mashindano ya Sayansi ,Teknolojia  na Ubunifu [MAKISATU] yanatarajiwa
kufanyika Machi,16 hadi 20 mwaka huu katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Akizungumza jijini Dodoma na waandishi wa Habari  mara baada ya kuwasilisha  mada maalum ya Mashindano hayo kwa wanahabari,Mkurugenzi idara ya Sayansi,Teknolojia na Ubunifu kutoka Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,Prof.Maulilio Kipanyula amesema mashindano hayo yanalenga kutambua wabunifu kutoka  kwenye makundi
saba.

Ameyataja makundi hayo kuwa ni  shule za msingi,shule za sekondari,vyuo vya ufundi stadi,vyuo vya kati ,vyuo vikuu,taasisi za utafiti  na maendeleo na wabunifu
kutoka mfumo usio rasmi huku lengo kuu likiwa ni kuibua,kutambua na kuendeleza ubunifu.

Prof.Kipanyula amesema mashindano hayo yamekuwa na Manufaa makubwa
kwani kutokana na mashindano hayo mwaka jana waliweza kuibuka washindi
60 ambapo wameendelezwa na kwa sasa wanajipatia kipato kutokana na ubunifu wao.

Kwa upande wake mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini  ,Wizara ya
Elimu,Sayansi na Teknolojia Sylvia Lupembe amesema kuwa  kwa mwaka huu
washiriki wabunifu waliojitokeza kushiriki mashindano hao ni 583  na
zoezi lilishafungwa huku tathimini ikiendelea kufanyika.

Kwa upande wake Mtaalam wa Fizikia ya Mionzi kutoka Wizara ya
Elimu,Sayansi na teknolojia,Edwin Konzo amesema hakuna ukomo wa
ushiriki kwenye ubunifu isipokuwa mbunifu anatakiwa kuja na ubunifu
mwingine maana ubunifu alioshiriki mwanzo utakuwa umeingizwa kwenye
kanzi data[Data base]huku akibainisha kuwa uchoraji nao ni ubunifu  .

Jumla  ya Washindi 21  katika makundi 7 yataibuka katika  Mashindano
hayo  ambapo Mshindi wa kwanza  atapewa tuzo ya Tsh.milioni
tano[5000,000],Mshindi wa pili milioni tatu[3000,000]mshindi wa tatu
milioni mbili[2000,000].

Ikumbukwe kuwa Mashindano ya MAKISATU yalianza mwaka jana na mwaka huu
uratibu wa Mashindano hayo ni Wyest&Ofisi ya Rais -TAMISEMI,tume ya
Taifa ya Sayansi na Teknolojia[COSTEC] Pamoja na VETA huku kaulimbiu
ni “Sayansi,Teknolojia,na ubunifu kwa uchumi wa viwanda huku Taasisi
61 zikithibisha kushiriki katika mashindano hayo.