Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene
(kushoto), akizungumza na mama aliyejifungua watoto watatu mapacha, Mariam Jonas, katika hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa. Simbachawene ameahidi kuwahudumia mapacha hao mpaka watakapo kuwa watu wazima. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene
akiwaangalia watoto mapacha watatu waliozaliwa Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa, Mkoani Dodoma. Kushoto ni Mama Mzazi wa watoto hao, Mariam Jonas. Simbachawene ameahidi kuwahudumia mapacha hao mpaka watakapo kuwa watu wazima. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene
(kushoto), akiagana na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya
Mpwawa, Dkt Hamza Mkingule, baada ya kufika hospitali hapo kuwaangalia watoto mapacha watatu waliozaliwa katika Hospitali hiyo, Mjini humo Mkoani Dodoma. Simbachawene ameahidi kuwahudumia mapacha hao mpaka watakapo kuwa watu wazima. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene
(kushoto), akiongozwa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mpwawa, Dkt Hamza Mkingule, kuingia wodi namba nane ya Hospitali ya Wilaya ya Mpwapwa, kumwangalia mama aliyejifungua watoto mapacha watatu waliozaliwa katika Hospitali hiyo, Mjini humo Mkoani Dodoma. Simbachawene ameahidi kuwahudumia mapacha hao mpaka watakapo kuwa watu wazima. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.