Home Mchanganyiko MAJUKWAA YA HAKI JINAI YA MIKOA YOTE YAZINDULIWA KITAIFA SINGIDA

MAJUKWAA YA HAKI JINAI YA MIKOA YOTE YAZINDULIWA KITAIFA SINGIDA

0

 Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Rehema Nchimbi aliyesimama akizindua
Jukwaa la Haki Jinai Mkoa wa Singida. Kushoto ni Mkurugenzi wa
Mashitaka(DPP) Nchini, Biswalo Mganga na kulia in Katibu Tawala Mkoa wa
Singida Dkt. Angerina Lutambi

 Picha ya pamoja  baina ya Mkrugenzi wa Mashitaka,(DPP) Biswalo Mganga
mwenye suti , Mkuu wa Mkoa wa Singida (mwwnye kilemba) anayefuata
Dkt.Angelina Lutambi  Katibu Tawala Mkoa wa Singida na wajumbe wa Jukwaa
la Haki Jinai Mkoa wa Singida Mara baada ya kuzinduliwa kwa Jukwaa hilo
la Mkoa

Baadhi ya  watumishi wa Umma Singida walioshiriki kwenye uzinduzi wa Jukwaa la Haki Jinai Mkoa wa Singida( Picha Zote na John Mapepele,Singida

1024×768

Normal
0

false
false
false

EN-US
X-NONE
X-NONE

/* Style Definitions */
table.MsoNormalTable
{mso-style-name:”Table Normal”;
mso-tstyle-rowband-size:0;
mso-tstyle-colband-size:0;
mso-style-noshow:yes;
mso-style-priority:99;
mso-style-qformat:yes;
mso-style-parent:””;
mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;
mso-para-margin:0in;
mso-para-margin-bottom:.0001pt;
mso-pagination:widow-orphan;
font-size:11.0pt;
font-family:”Calibri”,”sans-serif”;
mso-ascii-font-family:Calibri;
mso-ascii-theme-font:minor-latin;
mso-fareast-font-family:”Times New Roman”;
mso-fareast-theme-font:minor-fareast;
mso-hansi-font-family:Calibri;
mso-hansi-theme-font:minor-latin;
mso-bidi-font-family:”Times New Roman”;
mso-bidi-theme-font:minor-bidi;}
 

Na John Mapepele, Singida

Mkuu wa Mkoa wa Singida,
Dkt. Rehema Nchimbi amezindua Jukwaa
la Mkoa  la Haki  Jinai leo huku  Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) Nchini,  Biswalo Mganga  akisema kuwa
uzinduzi huu unafanywa  kitaifa
mkoani Singida  na kuelekeza  mikoa yote nchini kuzindua ili kusaidia  kupambana
na uhalifu wa kijina katika  mikoa
husika hivyo kupunguza mrundikano wa
mahabusu.

Dkt. Nchimbi amesema kuzinduliwa kwa Jukwaa hili kutakuwa
nguzo kuu ya kuzima uhalifu katika Mkoa wa Singida, huku akiwataka wajumbe
kutumia jukwaa hili  kufanya utatifi na
kutafakari kwa kina  ni  namna
gani bora ya kudhibiti uhalifu
badala  ya kusubili  utokee na kupeleka kesi mahakamani, jambo
ambalo amesema  madhara yake
yamekuwa  makubwa.

“Namshukuru Mungu. Leo, kwangu ni siku ya kihistoria na ya
kipekee ambayo  nilitamani  kuona inatimia  tangu siku nyingi. Kila wakati nimekuwa
nikiwasisitiza  kuwa ni muhimu na ni
lazima vyombo vyote vya Serikali katika mkoa wetu kufanya kazi ya
kupambana  na uhalifu kwa  pamoja
badala ya kila  mmoja kujiona  ni bora zaidi katika  nafasi yake jambo halina tija  na halitusaidii kama taifa, lakini hatimaye
leo hili linatimia” alisisitiza

Aidha amewataka Wajumbe kufanya kazi  kwa umoja
na uzalendo  ili jukwaa hilo liwe
mfano  bora na mikoa mingine  waje kujifunza.

“Kama  kwenye  mambo mengine tumeweza  kushika nafasi za kwanza  kitaifa kwa nini  tusiwe wa kwanza  katika
kufanya kazi  nzuri kwenye  kutekeleza majukumu ya jukwaa la Haki Jinai
kwenye Mkoa wetu na wengine waje kujifunza kwetu, inawezekana endapo kila mtu
atatekeleza wajibu wake” alisisitiza
Dkt. Nchimbi

Dkt. Nchimbi
amesema  hata vitabu
vitakatifu  vimeandika  mwisho ya
uhalifu ni mbaya  na kwamba  msharaha wa dhambi  ni mauti na kuelekeza kuwa kila  Ofisi
na Idara ya Serikali  katika Mkoa
wa Singida kuwa  na mfumo wa  Jukwaa la Haki Jinai ambao utasaidia
kujenga  mfumo wa kutafakari na kudhibiti
uhalifu badala ya kusubiri utokee.

Amesema ili kuwa na ufanisi na tija  wa kutokomeza uhalifu kwenye Mkoa wake
ameyataka  majukwaa ya Haki Jinai ya kila
Wilaya  kuanza mara moja  kufanya kazi na kupeleka mapendezo  yake
katika Jukwaa la Mkoa  kwa  kuwa  Jukwaa la Mkoa linategemea  utendaji wa
majukwaa ya Wilaya.

Akizungumza katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida
kabla  ya uzinduzi huo , Mganga amesema
kwa  mujibu wa Sheria ya Mashitaka  na 27 ya mwaka 2008 ibara  ya 59(B) (II) na  kwa mujibu wa Katiba ya Nchi, Mkurugenzi wa
Mashitaka ndiye mwenye jukumu la kuratibu upepelezi  wa kesi zote za jinai nchini japokuwa
anaweza  kukasimu madaraka hayo kwa
vyombo  vingine vya Serikali.

Amesema Ofisi  yake
imedhamilia  kutokomeza uhalifu wa
kijinai kwa  kutekeleza mkakati wa kuunda
kwa  majukwaa  ya Haki Jinai kila  Mkoa hapa nchini  ambalo
ni takwa la kisheria  ili
kuwa  muarobani wa kuthibiti   matukio na kesi za kijinai badala  ya kusubiri
makosa yafanyike na kutoa hukumu jambo ambalo amesema  halina tija
kwa  wananchi na taifa kwa ujumla.

Mganga amesema  kwa  kuzingatia
ukubwa wa  tatizo   na ongezeko wa uhalifu wa kijinai Serikali
ya Awamu ya Tano chini ya Rais, John Pombe Joseph Magufuli iliamua  kufanya marekebisho  makubwa ya kupambana na tatizo hili ambapo
iliunda  Ofisi ya Taifa  ya Mashitaka
kwa kutangaza  kwenye  gazeti la Serikali namba 49,  tarehe 13/2/2018 tofauti na awali ambapo  Kurugenzi ya
Mashitaka (DPP) ilikuwa chini  ya
Ofisi ya Mwanasherioa Mkuu wa Serikali.

Amewataka  wajumbe wote
wanaounda  jukwaa  hilo
kufanya kazi kwa weredi na kushirikiana
ili kuhakikisha mazingira ya
shughuli za kijinai yanakwenda vizuri ambapo amesema majukwaa  ya Mkoa yanatakiwa  kutoa mapendekezo ya  nini kifanyike  kwenye Jukwaa la Haki Jinai la Taifa kwa
ajili ya utekelezaji na ufuatiliaji.

Amesema kuliungana na Sheria ya Mashitaka, Jukwaa la Haki
Jinai la Mkoa linatakiwa kukaa vikao visivyopungua  viwili kwa
mwaka  ambapo amesisitiza   wajumbe kuhudhuria wao wenyewe badala ya
kuja wawakilishi kwa kuwa  sheria
inawataka wajumbe halisi na sio wawakilishi na kuongeza kuwa  kama kunakuwa na ulazima  au umuhimu, vikao hivyo  ninaweza
kuketi zaidi ya mara mbili kwa  mwaka kadri ya mahitaji.

Mkurugenzi, Mganga ameelekeza
Jukwaa la Haki Jinai Mkoa wa Singida  kuanza kazi mara mmoja  ili kutatua
changamoto mbalimbali zinazokabili
uhalifu katika mkoa ambapo amelitaka
kuketi  mara mbili kabla ya Oktoba
mwaka

Mwenyekiti wa Jukwaa la Mkoa wa Singida, Rose Chilongozi  ambaye ni Mwendesha Mashitaka Mkoa wa Singida
alimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Singida   kwa
kuzindua Jukwaa hilo na  kumhakikishia
kuwa yeye na wajumbe wake watafanya kazi kwa ushirikiano  mkubwa ili
kudhibiti uhalifu katika  mkoa
huo.

 Katibu wa Jukwaa la
Haki Jinai Mkoa wa Singida ambaye
ni  Mkuu wa Upelelezi Mkoa huo,
Kamishina Msaidizi wa Polisi, Stela  Mutabihirwa amewataja  wajumbe wa
Jukwaa hilo kuwa ni pamoja na Mwendesha Mashitaka wa Mkoa ambaye ni
Mwenyekiti, Mkuu wa upelelezi wa Mkoa ambaye ni Katibu, Mkuu wa Usalama wa
Taifa wa Mkoa, 
Wengine ni Afisa Ustawi wa Mkoa, Mwenyekiti wa  Bodi ya Parole  wa Mkoa, Afisa Mkemia Mkuu wa Mkoa,  Afisa-Bwana Huruma wa Mkoa, Mwanasheria
kutoka Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa na Afisa
wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa  na mdau mwingine yoyote ambaye wataona
anafaa  kumwalika  kushughulikia jambo husika.

Kamishina  Msaidizi wa
Polisi Mutabihirwa  ambaye  ni Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Singida
amesema  kwa upande wa Polisi anaishukuru
Serikali kwa kuharakisha kuzindua  jukwaa
hilo kwenye Mkoa wa Singida kwa kuwa litasaidia
kutatua changamoto mbalimbali za uhalifu.

“Napenda kumshukuru Mheshimiwa, Rais Magufuli kwa  kuunda
chombo  hiki kupitia Ofisi  ya Mashitaka
kwani kwa sisi Jeshi la Polisi tutashikisha dawati letu la  Polisi Jamii ambapo sasa  naamini
tutatoa elimu mashuleni na kupunguza mimba za utotoni pia uhalifu wa
mauaji,  ukatili wa kijinsia na migogoro
ya ardhi na mashamba  ya wananchi katika
Mkoa wetu itapata  ufumbuzi wa kudumu”
ameongeza  Afande Mutabihirwa  

Akifungua rasmi kikao cha uzinduzi wa Jukwaa hilo Katibu  Tawala wa Mkoa wa Singida Dkt. Angelina
Lutambi amesema  kila mwananchi anawajibu
wa  uzuia uhalifu  ili Mkoa wa Singida uwe sehemu salama.

Aidha aliwaasa wajumbe 
kufanya  kazi kwa kuzingatia
sheria  ili kuwa ukuta imara wakuzuia
aina yoyote ya uhalifu ambao unaweza kupenya 
na kuingia makao makuu ya nchi.