Home Michezo NIYONZIMA AIPELEKA YANGA ROBO FAINALI YA ASFC,AZAM FC NAYO YATINGA KWA MATUTA...

NIYONZIMA AIPELEKA YANGA ROBO FAINALI YA ASFC,AZAM FC NAYO YATINGA KWA MATUTA JIJINI MBEYA

0

………………………………………………………………………………………………….

Goli pekee la kiungo fundi Haruna Fadhili Niyonzima limewavusha Yanga hatua ya robo fainali ya michuano ya Azam Sports Federation CUP (ASFC) .

Yanga ikicheza kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam imeutumia vyema baada ya kuibuka na ushindi wa ba0 1-0 dhidi ya Gwambina FC kutoka wilayani Misungwi mkoani Mwanza.

Niyonzima amefunga bao dakika ya 45 kipindi cha kwanza akiachia shuti kali lililomshinda mlinda mlango wa Gwambina na kutinga wavuni

Licha ya Yanga kupata ushindi wamepata upinzani mkali toka kwa Gwambina FC inayocheza Ligi Daraja la kwanza ambayo imecheza mpira wa kitabuni na kuweza kuwazidi wenyeji kwenye umiliki wa mpira.

Yanga ambapo imefika hatua hiyo ya Robo Fainali haijaruhusu bao lolote kwenye Michuano hiyo tangu ianze.

Katika uwanja wa Sokoine mjini Mbeya Bingwa mtetezi wa Kombe hilo Azam FC imesonga mbele mara baada ya kuitoa timu ya Daraja la kwanza Ihefu FC kwa mabao 5-4 kwa mikwaju ya Penalti mara baada ya dakika 90 kumalizika bila kufungana.

Timu ambazo mpaka sasa zimeshatinga Robo Fainali ya Michuano hiyo ni Bingwa Mtetezi Azam Fc,Yanga SC,Simba SC,Namungo FC,Ndanda FC,Alliance FC,KMC FC na Sahare All Stars, timu 7 zikiwa za Ligi Kuu na Moja kutoka Ligi Daraja la kwanza.