Home Mchanganyiko NAIBU WAZIRI AWASHA UMEME KWENYE VIJIJI SITA MKOANI MTWARA

NAIBU WAZIRI AWASHA UMEME KWENYE VIJIJI SITA MKOANI MTWARA

0

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akisalimiana na viongozi mbalimbali wa kijiji Kipimi, kata Makota, Wilaya ya Newala, Mkoa wa Mtwara wakati akiwa kwenye ziara ya kazi ya ukaguzi wa kazi ya usambazaji umeme vijijini.

Wananchi wa kijiji cha Kikuyu, kata ya Mahumbika, Wilaya ya Newala, Mkoa wa Mtwara, wakifurahiya ujio wa Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu(hayupo pichani) kwenye kijiji chao.

Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu akiwapungua mikono kwa furaha wananchi wa kijiji cha Mmovo, kata ya Muungano, Wilaya ya Newala, Mkoani Mtwara wakati akiwa kwenye ziara ya kazi ya ukaguzi wa kazi ya usambazaji umeme vijijini.

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akiongea na wananchi wa kijiji cha Nakayaka (hawapo pichani) , Kata ya Chikongola, Wilaya ya Tandahimba, Mkoa wa Mtwara.

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akikata utepe kwenye nyumba ya MzeeJuma Siki Linjonda(Aliyeshika utepe) kuashiria kuwasha umeme katika Kijiji cha Kikuyu, kata ya Mahumbika, Wilaya ya Newala, Mkoa wa Mtwara.

Wananchi wa kijiji cha Tandika kata ya Dinduma, wilaya ya Tandahimba wakisikiliza Naibu Waziri wa Nishati(hayupo pichani) wakati akiwa kwenye ziara ya kazi ya ukaguzi wa kazi ya usambazaji umeme vijijini.

**************************

Hafsa Omar-Mtwara

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu jana Februari 25,2020 amewasha umeme kwenye vijiji sita vilivyopo katika Wilaya ya Newala na Wilaya ya Tandahimba,Mkoani Mtwara.

Vijiji hivyo ni pamoja na kijiji cha Kilidu,Mmovo,Kipimi,Kikuyu vilivyopo katika wilaya ya Newala, na vijiji vyengine viwili ni Nakayaka na Tandika ambavyo vipo katika Wilaya ya Tandahimba, Mkoani Mtwara

Akizungumza na waandishi wa habara, mara baada ya kuwasha umeme kwenye vijiji hivyo, Naibu Waziri alisema jitihada za Waziri wa Nishati kuwaita mara kwa mara wakandarasi wa miradi ya REA na kufanya nao vikao pamoja usimamizi mzuri wa TANESCO na REA imesaidia mkandarasi huyo kufanya kazi kwa haraka zaidi.

Aidha, amesema katika ziara yake hiyo Mkoani humo, kipindi hiki amepata matumaini kuona kazi za usambazaji umeme zinaenda vizuri ambapo wananchi wengi wameunganishiwa umeme na Mkandarasi huyo kuvuka idadi ya wateja iliyokuwepo, na kufurahishwa na kitendo cha wananchi wa vijiji hivyo kufurahi kupata huduma hiyo.

Alisema, kupatikana kwa wateja wengi katika miradi hiyo ni fursa kubwa kwa ya Wizara ya Nishati na taasisi zake zinazohusika na masuala ya umeme katika kuendeleza sekta hiyo.

“Miradi hii ikimalizika tutamkabidhi TANESCO na ukimkabidhi miundombinu ya miradi pamoja na wateja wengi wa kutosha wa mradi mzima huu utakuwa ni mtaji mkubwa kwa TANESCO, tunachotegemea sasa kutoka Tanesco ni kazi ya usambazaji maana tutakuwa tumemkabidhi mtaji wa wateja na miuondombinu maana yake tumemkabidhi fedha”

Alieleza kuwa, Serikali imejipanga kutoa huduma ya umeme wa uhakika katika Mikoa ya Mtwara na Lindi kwa kuzingatia hilo Serikali imechukua hatua mbalimbali za kuboresha kituo za kuzalisha umeme cha Mtwara kwa kukiongezea mashine mbili mpya ili kuweza kuhudumia kwa ufanisi.

“Wananchi wanataka umeme wa uhakika sio unamunganishia leo Kesho umeme unanza kukatika, baadhi wa wananchi vitu vyao vya thamani vinaungua,kama Serikali tumejipanga na tutahakikisha tunatoa umeme wa uhakika”Alisema Mgalu

Sambamba na hilo, pia amewatoa hofu watumiaji wa gesi nchini kwa kueleza kuwa Serikali ipo katika hatua ya mazungumzo ya kuhakikisha bidhaa ya gesi inayotumika majumbani inaagizwa kwa pamoja kama ambavyo ilivyofanyaa kwenye mafuta, ambapo tumepima mafanikio ya utaratibu huo imeweza kushusha bei ya mafuta kwasababu imeshusha gharama za uingizaji na kwa gesi tunafanya hivyo.

Alifafanua kuwa, kwa utaratibu wa uagizwaji Gesi pamoja itasaidi Gesi kuingia kwa wingi kwa pamoja nchini, ambapo itasaidia kukuwa kwa soko la Gesi na matumizi ya gesi yataoengezeka, na Serikali imejipanga kikamilifu kumuondoa mama kwenye matumizi ya kuni.