Home Mchanganyiko CHAURU YATARAJIA KUPATA SOKO LA UHAKIKA MSIMU HUU MPYA-CHACHA

CHAURU YATARAJIA KUPATA SOKO LA UHAKIKA MSIMU HUU MPYA-CHACHA

0
……………………………………………………………….
NA MWAMVUA MWINYI, PWANI
CHAMA Cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Mpunga Ruvu (CHAURU) ,uliopo Ruvu ,Chalinze mkoani Pwani ,kinatarajia kuondokana na kilio cha ukosefu wa soko la uhakika la mchele ,katika msimu wa mavuno 2020/2021 baada ya kupatikana mnunuzi kutoka nchini Uholanzi.
Aidha ushirika huo ,unalenga kuzalisha na kuinua mavuno kwa wakulima wake kutoka tani 4,700 walizopata msimu uliopita na kufikia tani 5,500 kwa mwaka huu.
Akielezea malengo ya msimu mpya wa kilimo cha mpunga, mwenyekiti wa ushirika wa CHAURU ,Sadala Chacha alisema ,mnunuzi huyo atanunua mchele kwa sh. 1,500-sh.2,000 kwa kilo .
Hata hivyo anabainisha ,wameahidi kuja kuangalia namna tunavyoandaa kilimo kabla ya kuingia mkataba “:”
Pamoja na hilo, Sadala alifafanua wakulima wameinua mavuno yao kutoka magunia 20 hadi gunia 80 ambapo msimu unaokuja mavuno yanaweza kupanda zaidi kutokana na kuwa na wataalamu wa kilimo.
Aidha alieleza,waliyumba baada ya pampu ya maji kuharibika kutokana na uchakavu hivyo waliikarabati kwa sh.milioni 50 fedha ambayo ilitokana na michango ya wakulima. 
“Tulikuta miundombinu ya umeme hakuna, tulikuwa tunatumia dizel kuendesha mtambo wa kusukumia maji, miundombinu ya mifereji ilikuwa chakavu lakini tumeweza kukomboa kinu cha kukobolea mpunga ambacho kwa miaka mingi kilikuwa kinamilikiwa kiujanja na Wachina”alieleza Sadala.
Mwenyekiti huyo ,alihimiza usafishaji wa mashamba na pia aliomba wenye matrekta kujitokeza kwani wanamahitaji ya matrekta hadi 50 kwa ajili ya kukimbizana na msimu huu.
Nae ,mmoja wa wanachama wa  ushirika huo ,Thomas Moler alisema wamenufaika na shamba hilo kwakuwa wanalima na kuuza hasa mchele ambao endapo unapata soko la kudumu manufaa yake ni makubwa.