Home Biashara Vodacom yafidia wateja kwa usumbufu kutokana na ukosefu wa Intaneti.

Vodacom yafidia wateja kwa usumbufu kutokana na ukosefu wa Intaneti.

0

****************************

Kama tulivyoahidi jana kufuatia kurejea kwa huduma ya Intaneti, tunaendelea kufidia wateja wetu waliopata usumbufu uliojitokeza baada ya kukosekana intaneti. Kwa mara nyingine tunapenda kuwashukuru wateja kwa uvumilivu wao. Tunawataarifu kwamba fidia  inatolewa kwa misingi ya ukweli na uwazi na itamfikia kila mteja aliyepata athari kama ifuatavyo: Kiwango cha chini kwa wateja wote wanaotumia huduma ya malipo ya kabla (Prepaid) ni Mbs 300 na wale wanaotumia huduma ya malipo ya baada (Postpaid) ni Mbs 600. 
Wale ambao vifurushi vyao vilifikia kikomo jana watapokea salio lao katika mfumo wa Mbs. Wale ambao walinunua kifurushi cha siku watapokea  kifurushi hicho pamoja na kifurushi cha nyongeza. Wale ambao walinunua vifurushi zaidi ya mara moja wakati hitilafu ilipotokea watarudishiwa pesa kwa njia ya muda wa maongezi au M-Pesa kulingana na mfumo waliotumia kununua vifurushi hivyo pamoja na kuongezewa kifurushi cha bure.
Tunawashukuru wateja wetu wote kwa kuendelea kuwa nasi. Tunaahidi kukamilisha zoezi hili leo, Februari 24, 2020
Imetolewa na Rosalynn Mworia, Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano, Vodacom Tanzania PLC.