Mshindi wa kwanza mita 100 wanawake, Win Makenji, kutoka Zanzibar,akimaliza mbio wakati wa mashindano yalioandaliwa na Shirikisho la Riadha Tanzania RT yaliofanyika katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam jana kusaka viwango vya kuunda timu ta Taifa ya Relay.
Mshindi wa kwanza mita 400 waume, Mohammed Ally kutoka Zanzibar,akimaliza mbio wakati wa mashindano yalioandaliwa na Shirikisho la Riadha Tanzania RT yaliofanyika katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam jana kusaka viwango vya kuunda timu ta Taifa ya Relay..
Mshindi wa kwanza mita 100=C2=A0 wanaume, Elias Selivester, wa Dar es Salaam akimaliza mbio wakati wa mashindano yalioandaliwa na Shirikisho la Riadha Tanzania RT yaliofanyika katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam jana kusaka viwango vya kuunda timu ta Taifa ya Relay.
MASHINDANO ya mwisho kuunda timu ya Taifa ya Mbio za Kupokezana Vijiti ‘Relays’ yamefanyika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam jana huku ikishuhudiwa wanaume wakifanya vema kuliko wanawake katika kufikia viwango vilivyowekwa na Shirikisho la Riadha Tanzania (RT).
Mashindano hayo yaliyokuwa ya kuhitimisha ‘trials’ mbalimbali zilizokwishatangulia mikoa mbalimbali, yalishirikisha wachezaji waliofikia viwango vilivyowekwa na Kamati ya Ufundi ya RT kutoka mikoa 11 ya Tanzania Bara na Visiwani, huku ikishuhudiwa ushindani mkali ukiwa kwa upande wa wanaume kuliko wanawake.
Lengo la mashindano hayo, ilikuwa kupata wachezaji wa kuunda timu za Relay mita 100X4 na 400X4.
Katika mbio za Mita 100 wanaume kulikuwa na ‘heats’ tatu ambako ya kwanza Joseph Williamalishinda akitumia sekunde 11.66 akifuatiwa na Amos Safari 11.96, Lazaro Charles 11.97 wa tatu huku nafasi ya nne ikienda kwa Samwel Msila 12.13 na wa tano Hussein Hamisi 12.55 wote kutoka Dar es Salaam.
‘Heat’ ya pili, Ali Hamis Gulam alishinda akitumia sekunde 10.40 akifuatiwa na Hassan Hamis 10.90 wote kutoka Zanzibar na watatu akaibuka Binamungu Katunzi wa Dodoma sekunde 10.91.
Nafasi ya nne ilikwenda kwa Jeremiah Baruti wa Dar es Salaam sekunde 11.70 wa tano Boaz Benesta wa Simiyu 12.08, wa sita Jacob Lugaila kutoka Mwanza 12.22 huku wa saba ni Fande Juma wa Singida sekunde 12.38.
Katika heat ya tatu wanaume, Elias Sylvesterwa Dar es Salaam alishinda akitumia sekunde 10.66 akifuatiwa na Abdallah Issa kutoka Zanzibar 10.72 huku nafasi ya tatu ikienda kwa Ismail Husseinwa Dodoma 10.91.
Nafasi ya nne ilikwenda kwa Selemani Kengwa wa Dar es Salaam 11.10 wa tano Daniel Mussa kutoka Mara 11.53 huku nafasi ya sita ni Japhet Kitugo wa Mara 12.05 na wa saba ni Ramachani Omari kutoka Singida sekunde 12.21.
Mita 400 Wasichana kukikuwa na ‘heat moja, ambapo ilishuhudiwa Jane Maiga wa Dar es salaamu akishinda baada ya kutumia sekunde 59.37 akifuatiwa na Theresia Benard Simiyu 01:00.41 akifuatiwa na Shuwena Mohamedi wa Dar es Salaam 01:04.69 huku Veronica Mlonge kutoka Iringa 01:05.62 na Halima Hamza wa Dar es Salaam akihitimisha kwa sekunde 01:10.92
Mita 400 Wanaume, Mohamedi Ally Mshambaalishinda akitumia sekunde 50.91 akifuatiwa na Simai Kombo Haji wote Zanzibar sekunde 51.41 wa tatu Twahil Haji Amer Dar Es Salaam 51.50.
Nafasi ya nne, Jeremiah Baruti akitumia sekunde 51.72, wa tano John Silima 51.88 wote kutoka Dar es Salaam wakati Boaz Benesta kutoka Simiyu alishika nafasi ya sita akitumia sekunde 52.16 na wa saba ni Matondo Magembe pia wa Simiyu 52.38.
Akizungumza mara baada ya mashindano hayo, Mjumbe wa Kamati ya Ufundi RT, Robert Kalyahe, alisema mashindano hayo ni hitimisho la agizo la Rais wa shirikisho, Anthony Mtaka, aliyeitaka na kuiwezesha mikoa kufanya mbio za majaribio kwa ajili ya kusaka wachezaji wa kuunda timu ya Taifa ya Relay kwa mita 100X4 na 400X4.
Alisema RT imeamua kuanza kugeukia mbio za uwanjani, baada ya muda mrefu nguvu kuwa ikiwekezwa kwenye mbio ndefu za barabarani.
Alisema wachezaji wengi wameonyesha ushindani, lakini hawakuweza kufikia viwango vilivyokuwa vimewekwa ambavyo ni sekunde 10.2 hadi 10.6 mita 100 na sekunde 46.5 hadi 47.4 mita 400 wanaume huku kwa wanawake mita 100 ni sekunde 11.4 hadi 12.5 huku mita 400 ni sekunde 52.00 hadi 58.6.
Kwa upande wake, Makamu wa Pili wa Rais RT-Ufundi, Dk. Hamad Ndee, aliwataka wachezaji kutokata tamaa bali wazidishe kujituma katika mazoezi huku nidhamu ndani na nje ya uwanja ikiwa kipaumbele.
Alisema kwa matokeo yaliyopatikana, angalau kwa wanaume hususa mita 100 waliokimbia chini ya sekunde 11 ambao ni sita wakiandaliwa ipasavyo wanaweza kufikia viwango vilivyokuwa vimewekwa na kuunda timu ya Taifa.
Dk. Ndee, alisema wanaandaa ripoti maalumu kwenda kwa Rais wa RT, ambapo watashauri wanariadha hao sita mita 100 wanaume waliokimbia chini ya sekunde 11, waingie kambini ili kuwanoa waweze kufikia malengo.