Home Mchanganyiko ‘LEADIMPACT UNIVERSITY’ YAWATUNUKU SHAHADA YA HESHIMA WATANZANIA, YUMO DC MJEMA

‘LEADIMPACT UNIVERSITY’ YAWATUNUKU SHAHADA YA HESHIMA WATANZANIA, YUMO DC MJEMA

0
 
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Dk. Sophia Mjema (katikati) akionesha cheti cha shahada ya heshima ya udaktari alichotunukiwa na Chuo Kikuu cha ‘LeadImpact’ (LeadImpact University) cha nchini Marekani kwa kutambua mchango wake katika kuihudumija jamii kwenye majukumu yake. Wa kwanza kushoto ni Mratibu wa Dawati la Jinsia na watoto Mkoa wa Kipolisi  Ilala, Afande Dk. Christina Onyango ambaye pia katunukiwa udaktari wa heshima na chuo hicho.

 

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Dk. Sophia Mjema akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kutunukiwa shahada ya heshima ya udaktari na Chuo Kikuu cha ‘LeadImpact’ (LeadImpact University) cha nchini Marekani kwa kutambua mchango wake katika kuihudumija jamii kwenye majukumu yake.


Mkuu wa Chuo Kikuu cha ‘LeadImpact’ cha nchini Marekani, Askofu Mkuu Cletus Bassey akizungumza katika hafla ya kuwatunuku shahada ya udaktari wa heshima  jijini Dar es Salaam.

 

Askofu Richard Harper toka Chuo Kikuu cha ‘LeadImpact’ cha nchini Marekani akizungumza katika hafla hiyo.

 

Mmoja wa wahitimu ambaye ni Mratibu wa Dawati la Jinsia na watoto Mkoa wa Kipolisi  Ilala, Afande Dk. Christina Onyango akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kutunukiwa udaktari wa heshima na chuo cha LeadImpact University cha nchini Marekani.

 

Mmoja wa watunukiwa wa shahada ya udaktari wa heshima toka LeadImpact University, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido, Dk. Jumaa Mhina akizungumza kukishukuru chuo hicho kwa kutambua mchango wa Watanzania hao kwa jamii.

 

Wanamahafali wa Chuo Kikuu cha ‘LeadImpact’ (LeadImpact University) wakiandamana kuingia katika Ukumbi wa Karimjee kutunukiwa…!

 

Brass Band ya Jeshi la Polisi ikiwaongoza Wanamahafali wa Chuo Kikuu cha ‘LeadImpact’ (LeadImpact University) kabla ya kutunukiwa…!

 

Sehemu ya wageni waalikwa katika mahafali hayo…
Mkuu wa Chuo Kikuu cha ‘LeadImpact’ cha nchini Marekani, Askofu Mkuu Cletus Bassey (kushoto) akimtunuku Mratibu wa Dawati la Jinsia na watoto Mkoa wa Kipolisi  Ilala, Afande Dk. Christina Onyango udaktari wa heshima.
Sehemu ya wanamahafali wa Chuo Kikuu cha ‘LeadImpact’ cha nchini Marekani wakiwa katika hafla hiyo.