Afisa Mhamasishaji wa Klabu ya Yanga Antonio Nugaz kulia akikabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Ngamiani Jijini Tanga Anjelina Mashaka kushoto kwa ajili ya wakina mama wajawazito wanaojifungua kwenye kituo hicho katikati anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa Mashindano wa Klabu ya Yanga Thabithy Kandoro
Afisa Mhamasishaji wa Klabu ya Yanga Antonio Nugaz kulia akikabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Ngamiani Jijini Tanga Anjelina Mashaka kushoto kwa ajili ya wakina mama wajawazito wanaojifungua kwenye kituo hicho leo katikati anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa Mashindano wa Klabu ya Yanga Thabithy Kandoro
Afisa Mhamasishaji wa Klabu ya Yanga Antonio Nugaz kulia akikabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Ngamiani Jijini Tanga Anjelina Mashaka kushoto kwa ajili ya wakina mama wajawazito wanaojifungua kwenye kituo hicho katikati anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa Mashindano wa Klabu ya Yanga Thabithy Kandoro
Afisa Mhamasishaji wa Klabu ya Yanga Antonio Nugaz kulia akikabidhi msaada wa vitu mzazi aliyemkuta kwenye wodi ya wakina mama wajazito kwenye Kituo cha Afya cha Ngamiani Jijini Tanga kushoto ni kwa ajili ya wakina mama wajawazito wanaojifungua kwenye kituo hicho leo katikati anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa Mashindano wa Klabu ya Yanga Thabithy Kandoro
Afisa Mhamasishaji wa Klabu ya Yanga Antonio Nugaz akizungumza mara baada ya kutoa msaada huo kulia ni Mkurugenzi wa Mashindano wa Klabu ya Yanga
Thabithy Kandoro
Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha
Ngamiani Jijini Tanga Anjelina Mashaka akizungumza huku akiishukuru Klabu ya Yanga kwa msaada huo
Mkurugenzi wa Mashindano wa Klabu ya Yanga Thabithy Kandoro akizungumza mara baada ya makabidhiano hayo kushoto ni Afisa Mhamasishaji wa klabu hiyo Antonio Nugaz
Afisa Mhamasishaji wa Klabu ya Yanga Antonio Nugaza kushoto akiwaongoza wanachama na wapenzi wa klabu hiyo kuingia kwenye kituo cha Afya Ngamiani Jijini Tanga kwa ajili ya kutoa msaada .
***********************************
KLABU ya Yanga imetoa msaada wa vitu mbalimbali kwenye wodi ya wakina mama wajawazito kwenye kituo cha Afya Ngamiani Jijini Tanga ikiwa ni mkakati wao kusaidia makundi mbalimbali kila wanapo kwenda kucheza mechi zao za ligi kuu ikiwa ni mpango wao wa kurudisha kwa jamii.
Msaada huo umekabidhiwa leo na Afisa Mhamasishaji wa Klabu ya Yanga Antonio Nugaz kwa Mganga Mfawidhi wa kituo hicho Anjelina Mashaka katika halfa iliyohudhuriwa mashabiki na wanachama wa timu hiyo mkoani Tanga.
Akizungumza wakati akikabidhi msaada huo Nugaz alisema wana mshukuru Mwenyezi Mungu amewawezesha kuwqa sehemu ambazo wazazi wao ambao walizaliwa kwenye vituo mbalimbali vya afy na wao wamefika kwenye kituo hicho kwa kile walichobarikiwa wakiotoe wodi ya wakina mama.
Alisema msaada ambao wameutoa pamoja na vitu vyengine lakini neti za kujikinga na mbu ambazo wamezikabidhi zitakuwa msaada mkubwa kwao ili kuepukana na kuumwa ugonjwa wa malaria.
“Wazazi ambao wamebahatika kupata watoto wanapaswa kujikinga na mbu ambao wanaeneza malaria hivyo katika kurudisha kwa jamii timu ya wananchi tumeona tuwasaidia neti na vitu vyengine ikiwemo sabuni na vifaa kwa ajili wa watoto wadogo”Alisema Mhamasishaji huyo.
Aidha alisema kwamba amefurahishwa na namna wanachama wa Yanga na mashabiki waliovyoonyesha mshikamano wa pamoja kwenye jambo hilo hivyo kwa niaba ya kamati ya utendaji chini ya Mwenyekiti wao Dkt Mshindo Msola na timu nzima.wanakwenda kuchukua pointi tatu ingawa mechi itakuwa ni ngumu.
Awali akizungumza katika halfa hiyo Mganga Mfawidhi wa kituo hicho Anjelina Mashaka aliishukuru klabu hiyo kwa kuona umuhimu wa kuwasaidia msaada huo ambao umefika wakati muafaka.
“Nashukuru kupokea neema ambazo mmezileta Yanga kwa niana ya Jiji la Tanga natoa shukrani zangu za dhati kwa ajili ya zawadi na wagonjwa wetu ambao wanajiandaa kupata watoto”Alisema Mganga huyo
Alisema kwamba pia wanathamini mchango wao wa kutoa sadaka kwap ambao utawasaidia kutokana na hapo awali kuwa na uhitaji wa neti ambazo zitasaidia kwenye kituo hicho.
Hata hivyo Mkurugenzi wa Mashindano wa timu ya Yanga Thabithy Kandoro alisema kwamba timu halisi ya Yanga lazima iende kwa vitendo ni jambo la msingi wao.