Home Mchanganyiko MASOKO YA KISASA NA YA MFANO KUJENGWA MWANZA

MASOKO YA KISASA NA YA MFANO KUJENGWA MWANZA

0

……………………………………………
 Shirika la kutetea haki za wanawake na wasichana KIVULINI la Jijini Mwanza kwa kushirikiana na Shirika la misaada kutoka Uingereza (I4ID) limeanza ujenzi wa masoko ya kisasa mkoani Mwanza yatakayokuwa mfano pia katika kuboresha masoko mengine nchini.

Akizungumzia ujenzi huo, Mkurugenzi wa Shirika la Kivulini Bw. Yasini Ally amesema, Masoko hayo yanajengwa katika maeneo ya Kiloleli Manispaa ya Ilemela na Mirongo jijini Mwanza yanahusisha miundombinu bora na rafiki ya kibiashara ikiwa ni pamoja na vyoo, eneo maalumu la kunyonyeshea watoto kwa wakina mama pamoja na Kituo cha daladala Kiloleli.

Soko la Kiloleli linatarajiwa kugharimu shilingi Milioni 127 huku soko la Mirongo likigharimu shilingi Milioni 90.8 ambapo ujenzi huo unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi mitatu kuanzia mwezi Februari 2020.