Home Mchanganyiko CCM YATOA SIKU 30 KUKAMILISHWA KWA MRADI WA MAJI KILINDINI – MICHEWENI,...

CCM YATOA SIKU 30 KUKAMILISHWA KWA MRADI WA MAJI KILINDINI – MICHEWENI, KASKAZINI PEMBA

0

………………………………………………………………………………………………….

Akiwa katika ziara ya kukagua na kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015 – 2020 katika Mkoa wa Kaskazini Pemba, Wilaya ya Micheweni, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi Ndugu Humphrey Polepole amesema Chama Cha Mapinduzi kimetoa siku 30 kukamilishwa kwa mradi wa maji Wilaya Micheweni Pemba.

Hatua hiyo imekuja baada ya Ndugu Polepole kufika katika eneo la Kilindini ambapo kuna chanzo cha maji kinachopasa kupeleka maji kwa kilometa 4.6 hadi eneo la Micheweni lakini mradi huo umekuwa ukisua sua kwa muda mrefu na kuelekeza kukamilika kwa haraka kwa mradi huo wa maji ili kurahisisha huduma za kijamii na Kiuchumi katika Wilaya ya Micheweni.