Home Mchanganyiko TAARIFA KWA UMMA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA

0

TAARIFA YA TUKIO LA KIFO LILILOTOKEA TAREHE 16.02.2020 KATIKA SHAMBA LA MIFUGO NA NYASI (NAFCO MABUKI) MALI YA SERIKALI / WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI LILILOPO KIJIJI CHA MABUKI WILAYA YA MISUNGWI BAADA YA KUVAMIWA NA KUWAJERUHI WAFANYAKAZI WA SHAMBA.

TAREHE 16.02.2020 MAJIRA YA 16:00 HRS HUKO KATIKA SHAMBA LA MIFUGO NA NYASI MALI YA SERIKALI / WIZARA YA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI (NAFCO MABUKI), LILILOPO KIJIJI / KATA MABUKI WILAYA YA MISUNGWI, MKOA WA MWANZA, WAFANYAKAZI WA SHAMBA HILO WAKIWA KWENYE KAZI ZAO ZA KILA SIKU WALIKAMATA MIFUGO 176 – NGO’MBE ILIYOINGIZWA NDANI YA SHAMBA LA SERIKALI NA WAFUGAJI KINYUME NA SHERIA, KANUNI NA UTARATIBU WA SHAMBA HILO.

BAADA YA MIFUGO HIYO KUZUILIWA, KUNDI LA WATU / WAHALIFU LILIJIKUSANYA (MOBILIZE) NA KWENDA KATIKA SHAMBA HILO  LA SERIKALI KWA NIA OVU YA KUCHUKUA KWA NGUVU MIFUGO HIYO ILIYOKAMATWA NA WALINZI / WAFANYAKAZI WA SHAMBA HILO. WAHALIFU HAO BAADA YA KUFIKA WALIANZA  KUWASHAMBULIA WAFANYAKAZI WA SHAMBA LA HILO KWA SILAHA ZA JADI ZIKIWEMO MAWE YALIYOKUWA YAKIRUSHWA KWA NJIA YA JADI @ makombeo NA HALI ILIPOZIDI KUWA MBAYA WAFANYAKAZI HAO WALIPIGA SIMU POLISI MISUNGWI ILI WAPEWE MSAADA WA KUOKOLEWA KUTOKA KATIKA MAZINGIRA YA KUUAWA.

JESHI LA POLISI BAADA YA KUPATA TAARIFA HIZO, WALIFIKA HARAKA KATIKA ENEO LA TUKIO KWA AJILI YA KUOKOA (RESCUE) NA KUREJESHA HALI YA USALAMA. HALI YA USALAMA ILIKUWA  MBAYA SANA NA WAHALIFU HAO WALIKUWA WAKIENDELEA KUWASHAMBULIA WAFANYAKAZI HUKU  WAFANYAKAZI WAWILI TAYARI WALIKUWA WAMEJERUHIWA VIBAYA KWA KUPIGWA MAWE KICHWANI NA MAENEO MBALIMBALI YA MIILI YAO KWA MAWE NA SILAHA ZENYE NCHA KALI KUTOKA KATIKA KUNDI HILO NA HALI ZAO ZILIKUWA MBAYA SANA.

ASKARI WA JESHI LA POLISI WALITOA ONYO / TAHADHALI LA KUTUMIA NGUVU KWA KUNDI HILO LA WAHALIFU KUWATAKA WAACHE MARA MOJA KUFANYA VURUGU NA KUHATARISHA USALAMA LAKINI WAHALIFU HAO WALIENDELEA KUKAIDI AMRI YA JESHI LA POLISI NA KUANZA KUELEKEZA MASHAMBULIZI KWA JESHI LA POLISI KWA KUWARUSHIA MAWE (MAKOMBEO). MAZINGIRA HAYO YALILAZIMISHA KUTUMIA NGUVU KUTULIZA VURUGU HIZO KWA KUTUMIA MABOMU YA MACHOZI 11.

LAKINI KUNDI HILO LILIKAIDI NA KUENDELEA KUWARUSHIA MAWE (MAKOMBEO) ASKARI HUKU WAKIWA NA NIA PIA YA KUWADHURU WAFANYAKAZI WA SHAMBA HILO, ILIBIDI ASKARI POLISI WALAZIMIKE KUJIHAMI KWA KUTUMIA RISASI ZA MOTO BAADA YA MMOJA WAO KUSHAMBULIWA KWA JIWE AMBAPO RISASI 03 ZILITUMIKA KWA AJILI YA KUOKOA MAISHA YA ASKARI ALIYEKUWA HATARINI NA KUOKOA MALI ZA SERIKALI NA WATUMISHI WA SHAMBA HILO WALIOKUWA WAMEUMIZWA SANA. RISASI 03 ZILIPIGWA HEWANI NA RISASI MOJA  ILIMJERUHI MHALIFU JOHN S/O LUGATA, MIAKA 30, MSUKUMA, MKULIMA NA MKAZI WA MANAWA ALIJERUHIWA KWENYE  MKONO WA KUSHOTO, JERAHA LILILOMSABABISHIA KUTOKWA NA DAMU NYINGI, KWANI WAHALIFU HAO WALIPOZIDIWA NGUVU NA POLISI WALIMBEBA NA KUONDOKA NAYE AMBAPO BAADAYE ALIFARIKI DUNIA WAKATI AKIPELEKWA HOSPITALI.

MAJERUHI HANGWA S/O MASANJA, MIAKA 28, MSUKUMA, MFANYAKAZI WA MABUKI FARM ALIJERUHIWA  SANA NA WAHALIFU HAO KICHWANI UPANDE WA SHAVU  NA SIKIO LA UPANDE WA KUSHOTO KWA JIWE LILILORUSHWA KWA KOMBEO, YEYE AMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA (W) MISUNGWI WODI YA WANAUME KITANDA NAMBA 03, HALI YAKE SIO NZURI. BENJAMIN S/O MUSSA, MIAKA 32, MSUKUMA, MKAZI WA MANAWA, MFANYAKAZI WA MABUKI FARM ALIJERUHIWA  SANA NA WAHALIFU HAO KICHWANI UTOSINI KWA KUKATWA NA KITU CHENYE NCHA KALI NA KUPIGWA MIGUU YOTE MIWILI KWA FIMBO, AMESHONWA NYUZI 06 KICHWANI, ALIPATIWA MATIBABU NA KURUHUSIWA KATIKA ZAHANATI YA MISASI.  PIA WALIJERUHIWA ASKARI NA. J. 2395 PC MAYANI AMBAYE ALIJERUHIWA KWA JIWE (KOMBEO) MKONO WA KULIA PAMOJA ANA ASKARI NA. H. 6418 PC MZEE ALIJERUHIWA KWA JIWE (KOMBEO) MKONO WA KULIA. ASKARI HAO WALITIBIWA NA KURUHUSIWA.

AIDHA, MIFUGO YOTE 176 – NG’OMBE IMELIPIWA FAINI YA SERIKALI KILA MFUGO TSHS. 100,000/= NA KUKABIDHIWA KWA WAMILIKI WA MIFUGO HIYO.

JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINATOA ONYO KWA WANANCHI WOTE WENYE TABIA ZA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KUWA WAACHE KWANI NI KINYUME NA SHERIA PINDI MTU / WATU WATABAINIKA HATUA KALI ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA  DHIDI YAO. SAMBAMBA NA HILO JESHI LA POLISI LINAOMBA WANANCHI WAENDELEE KUTOA USHIRIKIANO WA KUTOA TAARIFA ZA UHALIFU NA WAHALIFU ILI WAWEZE KUFIKISHWA MAHAKAMANI.