Home Michezo SIMBA YAJIWEKA KWENYE NAFASI NZURI YA KUTWAA UBINGWA WA LIGI KUU,YAICHAPA 1-0...

SIMBA YAJIWEKA KWENYE NAFASI NZURI YA KUTWAA UBINGWA WA LIGI KUU,YAICHAPA 1-0 KAGERA SUGAR

0

Goli pekee la Meddie Kagere alilotia kambani kwa mkwaju wa penati dakika ya 61 limetosha kuwapa Simba SC pointi tatu muhimu kuendelea kujikita kileleni mwa ligi .

Mchezo umemalizika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwa Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wageni Kagera Sugar kutoka mkoani Kagera.

Kwa matokeo hayo Simba imejiweka katika nafasi nzuri ya kutetea ubingwa wa Ligi Kuu bara kwa mara tatu mfululizo kutokana na watani zao Yanga dhahiri leo wamejiondoa kwennye kinyang’anyiro hicho kwa kulazimishwa sare na Polisi Tanzania.

Tazama hapo chini msimamo wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania bara.