Home Burudani JITIHADA ZA MAMLAKA YA USIMAMIZI WA WANYAPORI TANZANIA (TAWA) KUTANGAZA MALIKALE ZA KILWA...

JITIHADA ZA MAMLAKA YA USIMAMIZI WA WANYAPORI TANZANIA (TAWA) KUTANGAZA MALIKALE ZA KILWA ZAANZA KUZAA MATUNDA

0

Baadhi ya Kundi la Watalii wakiwa katika Eneo la Husini Kubwa -Kilwa Kisiwani

Meli iyowabeba watalii ikiwa imetia Nanga Kilwa Kisiwani

Watalii wakipokelwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Christopher Ngubiagai katika Gati ya Kilwa Kisiwani

Mhifadhi wa MaliKale za Kilwa chini ya Mamlaka ya Usimimizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA Mercy Mbogeleh  akizungumzia jitahada za TAWA katika kuhifadhi malikale za Kilwa chini ya Mamlaka hiyo.

Watalii wakiwa katika Matembezi ya Malikale za Kilwa Chini ya TAWA

                       ………………………………………………………………………………………….

WATALII Zaidi ya Mia tatu kutoka mataifa Mbalimbali Wamewasili kwa meli mbili na  kutembelea magofu ya Kilwa ambayo yapo chini ya Mamlaka ya usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA.

Wageni hao ambao walipokelwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilwa  Christopher    Ngubiagai walipata fursa ya kutembelea mali kale hizo ambazo zipo chini TAWA katika eneo la Kilwa Kisiwani,Wilayani Kilwa Mkoani Lindi.

Mkuu wa Wilaya ya Kilwa,Ngubiagai amewataka wananchi wa eneo wa Wilaya hiyo kuchangamkia fursa za kuwekeza katika sekta ya Utali kama wanavyofanya wakazi wa kanda ya Kaskazini

Amesema kuwa ni vyema wananchi hao kuwekeza katika sekta ya Hotel pamoja na vitu vya kitamaduni kwani hivi sasa kutakuwa idadi kubwa ya watalii wa ndani na nje ya Nchi kwani jitihada zinazofanywa na TAWA zimeanza kuzaa Matunda.

Kwa upande wake Mhifadhi wa MaliKale za Kilwa chini ya Mamlaka ya Usimimizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA Mercy Mbogeleh amesema kuwa watalii hao wamepata kutembelea Malikale hizo ambazo huwezi kuzikuta katika sehemu yeyote isipokuwa katika eneo la Kilwa

Aidha amewataka wananchi wa ndani na nje ya nchi kufika katika eneo hilo ili kuweza kujifunza historia ya Mji wa Kale ambao ulikuwa  ni maarufu kwa biashara ikiwemo vito vya thamani kama vile Dhahabu.

Nao Baadhi ya wananchi walisema kuwa hivi sasa watakuwa na fursa mpya za ajira katika Utalii jambo ambalo litasaidia kucha kutegemea uvuvi na kilimo katika kuendesha maisha yao.

Aidha wamesema kuwa toka TAWA imepewe usimamizi wa malikale hizo wameweza kunufaika kwa kupata boti hasa kwa wakazi wa eneo la Songomnara ambao walikuwa wakikabiliwa na adha ya usafiri huo hali iyowafanya kutegeme za wavuvi pekee.

Nao Baadhi ya watalii hao walionyesha furaha zao mara baada ya kutembelea eneo hilo na kusema kuwa watarudi kwa wakati mwingine ili kujifunza zaidi