Home Mchanganyiko MAZOEA YA KULIMA BILA  KUFUATA KANUNI BORA ZAWAPONZA WAKULIMA WA MAZAO YA...

MAZOEA YA KULIMA BILA  KUFUATA KANUNI BORA ZAWAPONZA WAKULIMA WA MAZAO YA BUSTANI MOROGORO

0

Naiman Molel Mtaalam wa Kilimo Kutoka Rijk Zwaan akionyesha Pilipili iliyotunzwa Vizuri kwa Wakulima.  

BAADHI ya Wakulima wakiwa Wanamsikiliza Mtaalam wa Kilimo Kutoka Rijk Zwaan Nahemia Gideon (mwenye Shati Jekundu) wakati wakipatiwa elimu ya Kisasa katika shamba Darasa la Kampuni hiyo Nanenane Mjini Morogoro

……………………………………………………

BAADHI ya Wakulima wa mazao ya Bustani Mkoani Morogoro  wamesema kuwa wamekuwa wakipata hasara katika Kilimo hicho kutokana na kulima kimazoea kwa kutofuata kanuni Bora za Kilimo hicho.

Wakulima hao wametoa Kauli hiyo wakati wakipatiwa mafunzo ya  ukulima wa kisasa juu mazao hayo ikiwa ni pamoja na nyanya pilipili hoho matango pamoja na mazao mengine ya jamii hiyo kutoka kwa Kampuni ya  Rijk zwaan Tanzania inayojishughulisha na Uuzaji wa mbegu bora za kilimo pamoja utoaji wa elimu ya Kilimo cha Kisasa katika maeneo mbalimbali ya Nchi ya Tanzania

Aidha Wakulima hao waliofika Katika kituo hicho cha Mafunzo Kilichopo ndani ya Viwanja vya maonyesho ya Kilimo Mjini Morogoro (nane nane) wamesema kuwa kutokana na elimu ambayo wamepatiwa hivi sasa watabadilika kwani Kilimo Cha hapo awali walikuwa wanitumia gharama kubwa huku faida yake ikiwa ndogo.

Wameeleza kuwa wanaamini elimu waliyopatiwa kutoka kwa wataalam hao itawakomboa hivyo kutoa wito kwa wakulima wengine kuweza kufika eneo hilo ili kupata elimu zaidi

Kwa upande wake Naiman Molel Mtaalam wa Kilimo Cha Kisasa kutoka Rijk zwaan Tanzania amesema kuwa hivi sasa wanatarajia kuona mabadilko makubwa kutoka kwa Wakulima hao Mara baada ya kuwapa elimu hiyo juu ya utumiaji wa mbegu Bora za Kilimo hicho.

Hata hivyo Naimani amesema kuwa wamekuwa wakitoa elimu hiyo Bure hivyo kuviomba vikundi vya Kilimo kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Morogoro na maeneo ya Jirani kufika katika kituo hicho ili kuweza kupata elimu zaidi jambo ambalo litasaidia kukuza uchumi wa mtu mmoja na Nchi kwa Ujumla.