Home Mchanganyiko RAIS DKT SHEIN AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI ZUNGU IKULU, ZANZIBAR

RAIS DKT SHEIN AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA WAZIRI ZUNGU IKULU, ZANZIBAR

0

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan Zungu (kushoto) akizungumza na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein alipomtembelea Ikulu ya Zanzibar leo wakati alipofanya ziara ya kikazi visiwani humo ambapo pamoja na mambo mbalimbali ametumia nafasi hiyo kujitambulisha kwa Rais Shein na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan akisalimiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein alipomtembelea Ikulu ya Zanzibar wakati wa ziara yake ya kikazi leo visiwani humo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan akiwa na mwenyeji wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein alipomtembelea Ikulu ya Zanzibar wakati wa ziara yake ya kikazi leo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akizungumza na Rais Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan ambaye alifika Ikulu ya Zanzibar leo ikiwa ni sehemu ya ziara yake visiwani humo leo. Wengine pichani ni viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na viongozi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na viongozi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo baada ya kukutana na kufanya mazunguzo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mussa Azzan aliyefika Ikulu kumtembelea ikiwa ni sehemu ya ziara yake.

(PICHA ZOTE NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)