Home Mchanganyiko TANZANIA KUKABILIANA NA MAGONJWA YA MILIPUKO

TANZANIA KUKABILIANA NA MAGONJWA YA MILIPUKO

0

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt.Zainabu Chaula akikagua sehemu maalumu ya kumpunzishia muhisiwa wa magonjwa ya milipuko kwenye mpaka wa rusumo mkoani kagera.

Maafisa afya wa mpaka wa rusumo wakitayarisha kifaa cha kupima joto la binadamu cha kutembea ambacho wasafiri kabla ya kuingia kwenye jengo hilo hupita na kufanyiwa uchunguzi.

Afisa afya Stanely Chipasula akimuelezea Katibu Mkuu jinsi utaratibu wa wanaoingia nchini wanavyofika eneo hilo huanza kunawa mikono.

Katibu Mkuu Dkt. Chaula akifanya ziara kwenye jengo la pamoja la idara zote zinazofanya kazi kwenye mpaka huo

Mgeni kutoka nchi ya Rwanda akinawa mikopo kabla ya kuingia ofisi ya afya.

Afisa Afya akiwa tayari kwa ajili ya kuwahudumia wasafiri kwenye mpaka huo

………………………………………………………………………………..

Na. Catherine Sungura-Kagera
Katika kukabiliana na magonjwa ya milipuko nchini wizara ya afya inajipanga kuboresha hali ya mipaka yake ili kuzuia magonjwa hayo yasiingie kwa kuboresha miundombinu ya kutolea huduma endapo itatokea muhisiwa.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula wakati wa alipotembelea mpaka wa manyovu mkoani kigoma na mpaka wa risumo mkoani kagera

“Tumefika mipaka hii kubwa ikiwa ni kuangalia utayari wetu wa kujikinga na maradhi haya ya kuambukiza ambayo yanaweza kuingia nchini”

Kwa upande wa manyovu katibu mkuu alibainisha mapunguvu ikiwemo ya eneo dogo hivyo kukubaliana kuweza kutatua mapungufu hayo ikiwemo namna ya kujenga jengo la pamoja na bora kwa huduma zote za mpaka huo.

“Tumeona eneo walilopo, wanakutana moja kwa moja na msafiri, ni dogo, watu wote wakishuka, wanaingia moja kwa moja mule ndani na kuonana na mtoa huduma,” alisema.

Aidha Dk. Chaula aliweza kuingia nchi ya Burundi na kuona jinsi walivyojiandaa alisema kwa upande wa Burundi ameona namna walivyojiandaa ikiwamo kuandaa hema maalum kwa ajili ya kuwaweka watu ambao watahisiwa kuwa na ugonjwa huo.

Hata hivyo alisema kuwa hapa nchini mambo makubwa yamefanyika, wataalamu wanafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha magonjwa haya hayaingii nchini, tumeongeza idadi ya watumishi mipakani hapa manyovu kutoka mmoja hadi watano, tumewapa pia vifaa vya ukaguzi na kujikinga lakini pamoja na juhudi hizi bado tuna changamoto zinatukabili ila watazifanyia kazi.

Sambamba na hilo, Katibu Mkuu huyo alifika pia katika eneo la na kujionea njia nyingi za mipaka isiyo rasmi ambapo wenyeji walimueleza wazi kwamba watu wa pande zote mbili (Tanzania na Burundi) huitumia kuingia na kutoka baina ya nchi hizo mbili.

Dk. Chaula alisema kupata ufumbuzi wa jambo hili, watajadiliana kwa kina na watendaji wa Wizara hizo mbili kupata ufumbuzi wa kuitatua changamoto hiyo, akitoa rai kwa watumishi wa afya kuendelea kutoa elimu kwa jamii, wajue namna bora ya kujikinga dhidi ya magonjwa hayo.

Kwa upande wa Rusumo Dkt.Chaula alisema ameridhishwa na utayari wa kukabiliana na magonjwa ambapo mpaka huo wana aina mbili za vifaa vya upimaji joto la binadamu ikiwepo ‘thermo scanner’ na ‘walk through’