Home Mchanganyiko DK MERU AMPONGEZA MURUSURI NA KUMTAKA KUKISAMBAZA AFRIKA KITABU CHAKE CHA “MAKING...

DK MERU AMPONGEZA MURUSURI NA KUMTAKA KUKISAMBAZA AFRIKA KITABU CHAKE CHA “MAKING AFRICA WORLD’S LARGEST ECONO

0
KATIBU MKUU Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi za Wakurugenzi za OSHA na VIPIMO (Weights & Measures), Dkt. Adelhelm Meru (Kushoto), akipokea
kitabu cha “MAKING AFRICA WORLD’S LARGEST ECONOMY” kutoka kwa mwandishi wa Kitabu hicho, Ndg. Derek Murusuri, jijini Dar es Salaam leo (13Feb.,
2020). Kitabu hicho cha kwanza kuihakikishia Afrika, pasina shaka kuwa inaweza kuongoza uchumi wa dunia, kilizinduliwa mwezi uliopita (January,
2020) na Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda.
 Dk. Meru ambaye  aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, na Mkurugenzi Mkuu wa EPZA, amempongeza Murusuri na kumtaka  akisambaze kitabu hicho katika mataifa mbalimbali ya Afrika ili kuleta hamasa na ari mya kwa waafrika waweze kuongeza juhudi na ubunifu katika kazi  ili kufikia uchumi shindani duniani. Amesema kitabu hiki kimekuja wakati mwafaka.