Home Siasa CHADEMA HOI IFAKARA

CHADEMA HOI IFAKARA

0

*********************************

13 Februari, 2020

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally, leo ameanza Ziara ya siku tatu Mkoani Morogoro ambapo katika mkutano wa ndani, madiwani watatu wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Ifakara wamejivua uwanachama wa Chadema na kujiunga na CCM.

Madiwani hao ni Mashaka Benard Mwenyekiti wa Halmashauri, Chiza Shungu diwani Kata ya Mbasa na Digna Nyangile diwani viti maalum Ifakara.

Viongozi hao wamejiunga na CCM leo tarehe 13 Februari, 2020 katika mkutano wa Katibu Mkuu na viongozi wa serikali na chama ngazi za mashina, matawi, kata, wilaya na mkoa wilayani Kilombero – Ifakara.

Wakati huo huo, Katibu Mkuu amekabidhi pikipiki kwa viongozi watendaji wa CCM wa kata za jimbo la Ifakara zilizotolewa na Mbunge wa Viti maalum Mama Getrude Lwakatare.

Aidha kabla ya mkutano huo, Katibu Mkuu ametembelea na kujionea mafanikio makubwa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM katika Sekta ya Afya kwa kukamilika kwa Hospitali ya kisasa ya Saratani ya Msamaria Mwema iliyojengwa na shirika la kimishionari la Huruma ambayo imegharimu shilingi bilioni 20.

Ziara hiyo imejumuisha viongozi wa Chama na serikali wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa Ndg. Innocent Kalogeris na Mkuu wa Mkoa huo Ndg. Loatha Sanare.

Ziara hii imelenga kuendelea kukiimarisha Chama katika ngazi za mashina, pamoja na kuendelea kujenga mahusiano mazuri baina ya viongozi ndani Chama, taasisi mbalimbali na serikali ili kurahisisha zaidi utolewaji wa huduma za maendeleo kwa wanananchi.