Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) akitoa salamu za pole kwa baadhi ya wafanyakazi wa Ubalozi wa Kenya Jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha Rais Mstaafu wa Kenya, Hayati Daniel Arap Moi
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) akisaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Kenya Jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha Rais Mstaafu wa Kenya, Hayati Daniel Arap Moi
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, wizara hiyo, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akisaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Kenya Jijini Dar es Salaam kufuatia kifo cha Rais Mstaafu wa Kenya, Hayati Daniel Arap Moi
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) pamoja na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Ubalozi wa Kenya Jijini Dar es Salaam mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo
…………………………………………………………………………………………….
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) pamoja na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge wamesaini kitabu cha maombolezo katika Ubalozi wa Kenya nchini kufuatia kifo cha Rais Mstaafu wa Kenya, Daniel Arap Moi aliyefariki 4 Februari, 2020.