1024×768

Normal
0

false
false
false

EN-US
X-NONE
X-NONE

/* Style Definitions */
table.MsoNormalTable
{mso-style-name:”Table Normal”;
mso-tstyle-rowband-size:0;
mso-tstyle-colband-size:0;
mso-style-noshow:yes;
mso-style-priority:99;
mso-style-qformat:yes;
mso-style-parent:””;
mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;
mso-para-margin:0in;
mso-para-margin-bottom:.0001pt;
mso-pagination:widow-orphan;
font-size:11.0pt;
font-family:”Calibri”,”sans-serif”;
mso-ascii-font-family:Calibri;
mso-ascii-theme-font:minor-latin;
mso-fareast-font-family:”Times New Roman”;
mso-fareast-theme-font:minor-fareast;
mso-hansi-font-family:Calibri;
mso-hansi-theme-font:minor-latin;
mso-bidi-font-family:”Times New Roman”;
mso-bidi-theme-font:minor-bidi;}
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt Rehema Nchimbi
(aliyeshika kisemeo) akiongoza mkutano
wa wadau wa elimu wa mkoa huo, kulia kwake ni Katibu Tawala wa Mkoa wa
Singida  Dkt. Angelina Lutambi,
anayefuata ni Afisa Elimu Mkoa wa Singida Mwalimu Nelasi Aron Mulungu

1024×768

Normal
0

false
false
false

EN-US
X-NONE
X-NONE

/* Style Definitions */
table.MsoNormalTable
{mso-style-name:”Table Normal”;
mso-tstyle-rowband-size:0;
mso-tstyle-colband-size:0;
mso-style-noshow:yes;
mso-style-priority:99;
mso-style-qformat:yes;
mso-style-parent:””;
mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;
mso-para-margin:0in;
mso-para-margin-bottom:.0001pt;
mso-pagination:widow-orphan;
font-size:11.0pt;
font-family:”Calibri”,”sans-serif”;
mso-ascii-font-family:Calibri;
mso-ascii-theme-font:minor-latin;
mso-fareast-font-family:”Times New Roman”;
mso-fareast-theme-font:minor-fareast;
mso-hansi-font-family:Calibri;
mso-hansi-theme-font:minor-latin;
mso-bidi-font-family:”Times New Roman”;
mso-bidi-theme-font:minor-bidi;}
Wanafunzi ambao ni wasichana rika  ndani shule za msingi katika kijiji cha Nkwae
katika Wilaya ya Singida DC  wakisubiri
kupokea fedha   jumla ya shilingi kwa
ajili ya mahitaji ya kishule ili kuepuka
vishawishi vinavyowafanya
washindwe kufanya vizuri kwenye
masomo yao kushoto ni Julius Nusu Kaimu Mratibu wa   Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF Wilaya ya
Singida akitoa maelekezo kwa wazee na wanafunzi


Na John Mapepele

“Mshike sana huyo elimu msimwache aende zake pia mtafute hadi
Uchina”  ni maneno aliyoyasema leo Mkuu
wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi katika kikao kazi cha wadau wote  wa elimu kwenye Mkoa wa Singida kutafakari ufaulu wa wanafunzi kwenye Shule
za Msingi na Sekondari  ambapo amesema  mkakati wa mwaka 2020  ni kwamba Mkoa wa wake lazima uwe
miongoni  mwa kumi bora.

Kwa mujibu wa Afisa Elimu Mkoa wa Singida, Mwalimu Nelasi
Mulungu  kwa matokeo ya mitihani ya mwaka
2019 Mkoa ulishika nafasi ya  22 kitaifa  kwa Shule za Msingi na  nafasi ya 21 kwa Kidato cha Nne na nafasi ya
2 kwa mitihani ya Kidato cha Sita.

Kikao kazi hicho kilikuwa na kauli mbiu “Timiza Wajibu Ongeza ufaulu”  ni cha aina yake kilicho washirikisha  wadau wote wa elimu ambapo Mkuu wa Mkoa  alisema
kuwa  kama Singida unaweza kushika
nafasi ya pili  kitaifa katika matokeo ya
kidato cha sita 2019 pia unaweza kushishika nafasi ya kwanza  katika mitihani yote kinachotakiwa ni
kutafakari  na kuweka mkakati wa pamoja
kwa wadau wote.

Dkt. Nchimbi ambaye pia kwa taaluma ni mwalimu aliyeanzia
shule za msingi hadi  vyuo vikuu vya
ndani na nje ya nchi alitumia muda mwingi kutoa maneno  kutoka
katika vitabu vitakatifu vya mungu vya Quran na  biblia akisisitiza kuwa   vitabu hivyo vyote  vimesisitiza
kuitafuta kwa bidii elimu  ambapo
alisema wadau wa elimu wanapaswa  kutafakari  kwa kina
ni kwa nini elimu imeendelea kushuka katika mkoa huo wakati wao wana
wajibu na kwamba kutowafaulisha watoto
ni dhambi kubwa.

“Nasema kwa dhati ya
moyo wangu  uchina  katika dunia hii ni Singida watu wanatakiwa
kutoka mataifa yote kuja kutafuta elimu hapa kwetu na watu wa kuifanya  iwe Uchina ni nyie”alisisitiza Dkt Nchimbi 

Katika kikao hicho Dkt nchimbi alikataa utaratibu wa kawaida
wa  kikao wa kuanza kusoma taarifa  za maendeleo ya elimu  na badala yake akaelekeza  kuanza
na ajenda ya kila mshiriki kueleza
nini kifanyike ili kuboresha ufaulu wa wananfunzi.

Alisema  kutokana na
kile alichokiita  dhambi ya baadhi ya
walimu kutotekeleza wajibu wa kutoa elimu
kwa kijituma  Mungu amekuwa  akiwaadhibu na kujikuta wanapata matatizo
makubwa ya kiuchumi na kijamii.

“Mungu anatoa adhabu hapa hapa duniani   baadhi ya walimu wanaacha kuwafundisha
watoto kwa bidii unakuta waingia mikopo kwa wakopeshaji haramu  ambao wana wakopesha milioni tatu wanalipa
milioni ishirini na ATM kadi zao zinachukuliwa na hao matapeli” aliongeza Dkt.
Nchimbi.

Hatimaye Mkuu wa Mkoa akapiga marufuku tatu ili kunusuru  kushuka kwa ufaulu katika mkoa wake.

Alipiga marufuku kwa wakopeshaji haramu kuendelea
kuwakopesha  walimu ambapo aliwaelekeza
wakuu wote wa wilaya kwenye Mkoa wa Singida kuanzisha operesheni maalum ya
kuwasaka wakopeshaji haramu na kuwachukulia hatua kali za kisheria.

Aidha alipiga marufuku kwa kwa wenye mabanda ya kuonyeshea
video kuwaingiza wanafunzi  na kutaka Kamati
za Ulinzi na Usalama za kila wilaya kuwakamata
wenye  vibanda ambapo alisema  hakuna yeyote anayevunja sheria
atakayepona  na kwamba wazazi  wanafunzi wanaoshinda kwenye mabanda hayo
watafuatiliwa kikamilifu ili pia sheria ichukue mkondo wake  kwa kuwa nao ni wadau wakuu katika kuhakikisha
kuwa watoto wao wanahudhuria masomo kikamilifu..

Marufuku ya mwisho ilikuwa katika suala la wanafunzi kucheza
michezo ya kamali
katika
nyumba za starehe  ambapo
alisema  nyumba  ziutakazobainika zikiwaingiza wanafunzi
zitachukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kufungiwa biashara hizo.

Awali kwa upande wake Afisa Elimu Mkoa wa Singida Mwalimu, Nelasi
Mulungu  kipaumbele cha Mkoa ni kuongeza
ufaulu katika mitihani yote, kuboresha miundombinu, kupambana na utoro,
kuongeza samani na kuboresha ufundishaji katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Kwa Mujibu wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ya mwaka 1995 kila shule ya
msingi ni lazima iwe na darasa la awali.  
 Hivyo Mkoa una jumla ya madarasa ya awali 536 kwa upande wa shule
za Serikali na shule 30 za awali zisizo za Serikali.

Amesema, Mkoa wa Singida una shule za msingi 569
kati ya hizo shule 536 ni za Serikali na shule 33 ni za Watu
binafsi, Taasisi na Mashirika ya Dini.
Kwa shule za msingi hali halisi ya mahitaji ya Walimu Kimkoa ni 9,885
ikilinganishwa na waliopo 5,292 sawa na asilimia 53.5. Upungufu
wa Walimu wa shule za msingi ni 4,593.

Kwenye matokeo ya kuhitimu elimu ya msingi ufaulu
umekuwa ukiongezeka sambamba na idadi ya wanafunzi kwa kila Halmashauri hivyo
kwa mwaka 2017 wanafunzi waliofaulu ni 17,863, mwaka 2018 ni 20,617 na mwaka
2019 ni 22,484.

Katibu Tawala Mkoa wa Singida  Dkt. Angelina Lutambi alisema  katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya
awamu ya Tano chini ya Rais John Pombe Joseph Magufuli imetoa zaidi ya bilioni
50 katika eneo  la elimu  pekee na kwamba  fedha hizo ni nje ya mishahara ya walimu.

Alisema  walimu
na wadau wote wa elimu wanapaswa
kushirikiana  ili kuinua kiwango
cha ufaulu kwa kuwa Serikali tayari imeshatekeleza wajibu wake wa kuwawezesha
kwa kiasi kikubwa.

Alipongeza jitihada za Mhe. Rais  Magufuli za kuwezesha  kwenye sekta mbalimbali ambapo alisema  uwezeshaji umekuwa wa kiwango cha juu
kinachotakiwa kufanyika kwa sasa ni watumishi wa Serikali kuunga mkono juhudi hizi
kwa vitendo.

Alisema kauli mbiu ya mwaka huu ya “Timiza Wajibu
Ongeza ufaulu” ndiyo mwongozo na dira
katika Sekta ya Elimu kwenye Mkoa wa Singida hivyo bila kutimiza wajibu
wa kila mdau nhakutakuwa na ufaulu wowote
na kuwataka walimu kusimamia viapo vyao.