Home Mchanganyiko MGUMBA AHIMIZA WAKULIMA KUPANDA MAZAO YA MUDA MREFU

MGUMBA AHIMIZA WAKULIMA KUPANDA MAZAO YA MUDA MREFU

0

Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki ambae pia ni naibu waziri wa Kilimo Omary Mgumba Alazimika kufanya mkutano usiku ili kusikiliza kero za wananchi wa Kijiji cha Magere Halmashauri ya Wilayani Morogoro

DSC_1525.JPG
Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mgumba akipokelewa kwa Ngoma Kijiji cha Magere Mkoani Morogoro
DSC_1536.JPG
Wananchi wa Magere wakiwa tayari Kumsikiliza Naibu waziri wa Kilimo Omary Mgumba
DSC_1538.JPG
  Wananchi wa Magere wakiwa tayari Kumsikiliza Naibu waziri wa Kilimo Omary Mgumba
…………………………………………………………………………………………………………..

NAIBU waziri wa Kilimo Omary Mgumba amewataka Wakazi wa Kata ya Kidugalo Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro,Mkoani Morogoro kujikita katika uzalishaji wa mazao ya muda mrefu ili kuepuka kuwa tegemezi pale wanapokuwa hawana nguvu za uzalishaji wa mazao ya muda mfupi

Mgumba Ambae ni Mbunge wa jimbo la Morogoro Kusini Mashariki ametoa kauli hiyo  wakati akiwa katika ziara ya Kijimbo ambapo alipata Fursa ya kutembelea Vijiji Vinne katika Kata hiyo.

Aidha Amesema kuwa anatambua juhudi zinazo onyeshwa na wakulima wa kata hiyo katika kuzalisha mazao ya muda mfupi ikiwemo mihogo,ufuta na mahindi.

Amesema sasa umefika wakati wa wakazi hao kuwekeza katika mazao ya Muda mrefu hasa zao la korosho kutokana na ardhi ya kata hiyo kuwa  nzuri yenye kukubali zao la korosho ambalo linafaida kubwa pale litakapotunzwa vizuri

Sanjari na hayo Naibu  waziri wa Kilimo Omary Mgumba amewataka Wakazi wa Kata hiyo ya Kidugalo Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro,Mkoani Morogoro kujikita katika uzalishaji wa zao la mihogo kutokana fursa nyingi katika zao hilo.

Amesemakuwa ili zao hilo kuwa na faida kubwa ni wajibu kwa wakulima kufuata kanunu bora la kilimo ili kuzalisha kwa tija kwani serikali ya awamu ya tano imefanikiwa kupata soko la mihogo katika nchi ya China.

Katika mikutano hiyo amewataka maafisa kilimo kuwatembelea wakaulima na kuwapatika elimu nzuri juu ya uchagua wa zao hilo ili kuepuka kutumia mbegu zisokuwa bora pamoja na kuwa mashamba darasa ya mazao mbalimbali.

Nao baadhi ya wakulima wa Vijiji hivyo wametoa pongezi zao kwa Naibu waziri huyo kutokana elimu ambayo amekuwa akiwapatia kila mara anapopata nafasi ya kukutana nao

Wamesema kuwa watazingatia elimu waliyoipata huku pia wakimuomba kusaidia kutatua migongano iliyopo baina ya wakulima na wafugaji hali ambayo imekuwa ikiwakatisha tamaa katika katika uzalisha wa mazao.

Akijibu hoja hiyo Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki ambae pia ni naibu waziri wa Kilimo Omary Mgumba ameyataka makundi hayo kuheshimu ya sharia,pamoja kuwa kamati za maridhiano jambo amablo litasaidia kuondosha migogoro.

Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki ambae pia ni naibu waziri wa Kilimo Omary Mgumba February 10,amefanikiwa kufanya mikutano ya hadhara katika vijiji vinne vya kata ya Kidugalo ambavyo ni Seregete A na B,Magera pamoja na Lubumu ambapo alipata kusikiliza kero mbalimbali za wananchi katika vijiji hivyo.

Hata hivyo wananchi hao walipata kuelezwa miradi mbalimbali ambayo serikali ya awamu ya tano imeitekeleza na inayoendelea kutelezwa katika kata hiyo ikiwemo,ujenzi wa vyumba vya madarasa,miradi ya maji pamoja na afya.