Home Michezo BARCELONA,REAL MADRID ZATUPWA NJE KOMBE LA MFALME

BARCELONA,REAL MADRID ZATUPWA NJE KOMBE LA MFALME

0

Wachezaji wa Barcelona wakiwa hawaamini macho yao baada ya kuchapwa 1-0 na Athletic Bilbao bao pekee la mshambuliaji Mspaniola, Inaki Williams mwenye asili ya Ghana dakika ya 90 , sekunde chache baada ya Lionel Messi kukosa bao la wazi kwenye mchezo wa Robo Fainali Kombe la Mfalme usiku wa jana Uwanja wa San Mamés Barria mjini Bilbao, hivyo kutolewa kwenye michuano hiyo PICHA ZAIDI SOMA HAPA  

Kiungo wa Real Madrid, Federico Valverde (kushoto) akisikitka baada ya mshambuliaji Alexander Isak kuifungia Real Sociedad mabao mawili dakika za 54 na 56 katika ushindi wa 4-3 dhidi ya wenyeji kwenye mchezo wa Robo Fainali Kombe la Hispania usiku wa jana Uwanja wa Santiago Bernabeu Jijini Madrid. Mabao mengine ya Real Sociedad yalifungwa na Martin Odegaard dakika ya 22 na Mikel Merino dakika ya 69, wakati mabao ya Real Madrid yalifungwa na Marcelo dakika ya 59, Rodrygo dakika ya 8 na Nacho dakika ya 90 na ushei PICHA ZAIDI SOMA HAPA