Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle akizungumza na mameneja (hawapo pichani) wakati wa kikao cha mapitio ya taarifa ya utendaji kazi wa nusu mwaka kwa mwaka wa fedha 2019/2020 kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha. Kulia ni meneja wa TEMESA mkoa wa Arusha Mhandisi Heriel Mteri na kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Vivuko Mhandisi Adelard Kweka.
Baadhi ya mameneja wa mikoa na vituo wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA waliohudhuria kikao cha mapitio ya taarifa ya utendaji kazi wa nusu mwaka kwa mwaka wa fedha 2019/2020 wakisikiliza kwa umakini taarifa mbalimbali zilizokuwa zikitolewa wakati wa kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha.
Meneja wa Uchumi kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Frederick Gwanchele akisoma taarifa kwa mameneja wa vituo na mikoa wa Wakala huo wakati wa kikao cha mapitio ya taarifa ya utendaji kazi wa nusu mwaka kwa mwaka wa fedha 2019/2020 kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha.
Mameneja wa mikoa na vituo wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) wakiwa katika picha ya pamoja na Mtendaji Mkuu wa Wakala huo Mhandisi Japhet Maselle (katikati) mara baada ya kumaliza kikao cha mapitio ya taarifa ya utendaji kazi wa nusu mwaka kwa mwaka wa fedha 2019/2020 kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha.
PICHA ZOTE NA TEMESA (ARUSHA)