Home Mchanganyiko UJENZI WA VYOO KATIKA BAADHI YA SHULE  HALMASHAULI YA BUKOBA VIJIJINI BADO...

UJENZI WA VYOO KATIKA BAADHI YA SHULE  HALMASHAULI YA BUKOBA VIJIJINI BADO NI  CHANGAMOTO.

0

**************************

BUKOBA,KAGERA.
NA SILVIA MCHULUZA.

Katika mwaka wa fedha 2019\2020 halmashauri ya wilaya ya bukoba vijijini imekumbwa nachangamoto ya ujenzi wa vyoo katika baadhi ya shule za msingi na sekondali ikiwa hayo yamebainishwa katika baraza la madiwani la halmashauli hiyo lililofanyika katika kata ya kemondo katika shule ya sekondali kashozi ikiwa ni kikao cha kwanza tokaea kuwepo kwa uhamaji wa halmashauli kutekeleza majukumu katika maeneo husika.

Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwa afisa mipango wa halmashauli Bw. Julian Talimo hiyo wakati akiwasilisha rasimu ya bajeti ya mwaka wa fedha 2020\2021 ambapo amesema katika mwaka huu wa fedha changamoto hii ya uabawa vyoo itatatuliwa kulingana na fedha inayotalajiwa kurasimishwa katika halmashauri  ambapo zaidi ya abilioni 56 na zaidi inategemewa kurasimishwa huku bilioni 5.8 inatarajiwa kwenda kwenye miradi vipolo na ujenzi wa halmashauli mpya  huo ukiwa ni mwongozo uliotolewa na wizara.

Hata hivyo nae mwenyekiti wa halmashauli ya wilaya ya bukoba vijijini mh. Murshid Ngeze ameongeza kwa kuwapongeza watunishi na madiwani kwa ujumla kutokana na halmashauli hiyo kupokea hati safi zaidi ya mala mbili lakini pia ametoa agizo kwa watendaji wa vjijiji kuhakikisha wanafanya kazi kwa juhudi ili kwenda na kasi ya awamu yatano.

Aidha ameongeza kwa kuzungumzia changamoto ambazo zipo katika halmashauri ikiwemo miundombinu mibaya ya barabara pamoja na changamoto ya umeme vijijini kutokana na kuwepo kwashirika la kusambaza umeme vijijini REA kuomba kuhakikisha wanatatua kero hiyo ili kuwapatia umeme wananchi ili kuleta maendeleo zaidi.

“changamoto ya umeme na maji tunatakiwa kuhakikisha inatatuliwa ili kuweza  kuleta maendeleo zaidi kwa wananchi ambapo tunatakiwa kushirikiana na wataalamu kama ni barabara basi tuwausishe TARURA umeme basi REA nao wahusike ili kuondoa changamoto hizi”Alisema Mh. Ngeze.

Sambamba na hayo afisa mipango Bw.Julian Talimo akuishia hapo aliweza kuwasilisha mipango ambayo imefanyika kwa mwaka fedha 2019/2020  kwa upande wa elimu msingi na sekondali ambapo halmashauli ilitegemea kuandikisha wanafunzi wa awali ni jumla ya 11933 ikiwa asilimia 79%  ya wanafunzi 15141 ndiyo iliyotarajiwa huku elimu maalumu zaidi ya wanafunzu 37 waliandikishwa katika vitengo viwili vya halmashauli.