Home Mchanganyiko Miili ya Askari 3 Yaagwa Njombe

Miili ya Askari 3 Yaagwa Njombe

0

*********************************

NJOMBE

Mamia ya watu wamejitokeza kuaga miili ya askari 3 walifariki katika ajali iliyotokea februari 3 majira ya saa kumi na mbili na robo katika mlima wa polisi mjini Njombe ambayo ilihusisha basi la abiria kampuni ya Sharon lenye nambari za usajiri T349 CXB na gari la polisi lenye nambari za usajiri PT 3734.

Miili iliyoagwa ni Michael Mwandu(24) ambao unapelekwa Geita,Marianus Hamis(27) Lindi pamoja na  Hery Athuman(31) ambao unapelekwa mkoani Kilimanjaro .

Akizungumza wakati wa kuaga miili hiyo katika viwanja vya polisi mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olesendeka pamoja na kamanda wa jehsi la polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa wanasema taifa limepoteza nguvu kazi ambayo ilikuwa katika utekelezaji wa majukumu ya taifa na kudai kwamba vyombo vya ulinzi na usalama vinafanya uchunguzi wa kina kujua kama kuna uezembe ulisababisha vifo ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.

Awali akingoza ibada ya kuombea marehemu hao askofu mkuu wa KKKT dayosisi ya kusini DR George Fyavango anasema vitaja hao wamefanya kazi iliyotuka enzi za uhai wao hatua ambayo imeligusa kila kundi katika jamii na kuwataka wanadamu kujiandaa na maisha baada ya kifo.

Kufuatia vifo hivyo vya askari watatu kati ya 12 waliokuwemo katika gari ya polisi wakielekea maeneo yao ya lindo , Baadhi ya wasafiri na wamiliki wa vyombo vya moto wamekuwa na maoni ili kuongeza usalama katika matumizi ya barabara 

Baada ya kutokea ajari hiyo inaelezwa dereva wa basi alitokomea kusiko julikana na kulifanya jeshi la polisi kuendelea kumtafuta  huku wengine wawili wakiendelea kupatiwa matibabu MOI.