Home Michezo KLABU YA SIMBA YAZIDI KUJIKITA KILELENI, YAINYUKA POLISI TANZANIA 2:1 TAIFA

KLABU YA SIMBA YAZIDI KUJIKITA KILELENI, YAINYUKA POLISI TANZANIA 2:1 TAIFA

0

***************************

NA EMMANUEL MBATILO

Klabu ya Simba imefanikiwa kuitungua timu ya Polisi Tanzania mabao 2:1 katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam huku ikiendelea kujiwekea rekodi kibao kwenye ligi.

Polisi Tanzania walianza kufunga bao lililopachikwa kipindi cha kwanza na nyota wa Polisi Tanzania Sixtus Sabilo dakika ya 22 na Simba ilisawazisha dakika ya 56 kupitia kwa John Bocco.

Ibrahim Ajibu alifunga bao la ushindi dakika ya 94 akimalizia pasi ya Francis Kahata.