Home Mchanganyiko WAZIRI SIMBACHAWENE, KATIBU MKUU KADIO WAWASILI OFISI NDOGO YA WIZARA DAR, WAZUNGUMZA...

WAZIRI SIMBACHAWENE, KATIBU MKUU KADIO WAWASILI OFISI NDOGO YA WIZARA DAR, WAZUNGUMZA NA WATUMISHI

0

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kushoto) akimsalimia Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ramadhani Kailima, wakati alipokuwa anawasili ofisi ndogo za Wizara, jijini Dar es Salaam, leo. Simbachawene na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio waliwasili katika ofisi hiyo baada ya Katibu Mkuu kuapishwa Ikulu, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio akiongozwa na Naibu Katibu Mkuu, Ramadhani Kailima (kulia), wakati alipokuwa anawasili ofisi ndogo za Wizara, jijini Dar es Salaam. Kadio aliwasili ofisini hapo baada ya kuapishwa Ikulu,jijini humo leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio (kulia) akiwasalimia Watumishi wa Idara ya Huduma kwa Wakimbizi wakati alipokuwa
anawatembelea ofisini jijini Dar es Salaam. Kadio aliwasili ofisi ndogo ya Wizara jijini humo, baada ya kuapishwa Ikulu, leo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kulia) akimsalimia Mtumishi wa Wizara hiyo, Edaline Osima, ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es
Salaam, leo. Simbachawene na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio waliwasili katika ofisi hiyo baada ya Katibu Mkuu huyo kuapishwa Ikulu. Picha
na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akimfafanulia jambo Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio (kushoto), na Naibu Katibu
Mkuu, Ramadhani Kailima (kulia), katika kikao kilichofanyika ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam, leo. Simbachawene na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,
Christopher Kadio waliwasili katika ofisi hiyo baada ya Katibu Mkuu huyo kuapishwa Ikulu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio (kulia) akiwasalimia Maafisa wa Idara ya Huduma ya Uangalizi na Probesheni wakati alipowatembelea ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam, leo. Kadio aliwasili katika ofisi hizo baada ya kuapishwa Ikulu. Picha na Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi.