Postamasta Mkuu, Hassan Mwang’ombe akizungumza wakati akimkaribisha Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe.
Mwakilishi wa Katibu Mkuu wizara hiyo (Sekta ya Mawasiliano), Kitolina Kippa akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
Waziri Mhandisi Kamwelwe (katikati), akizungumza na wajumbe wa Bodi hiyo, pamoja na Menejimenti ya Shirika wakati uzinduzi huo.
Mwenyekiti wa Bodi mpya ya Shirika la Posta (TPC), Kanali Mstaafu, Dkt. Haruni Kondo (kulia), akiwa na Postamasta Mkuu, Hassan Mwang’ombe (wa pili) pamoja na baadhi ya wajumbe wa bodi hiyo, wakipiga makofi wakati wa uzinduzi huo.
Baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Shirika la Posta wakimsikiliza Waziri alipokuwa akizungumza.
Baadhi ya Wajumbe wa Bodi mpya ya Shirika wakifuatilia shughuli mbalimbali zilizokuwa zikiendelea katika uzinduzi.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akizungumza wakati wa uzinduzi.
Mwenyekiti wa Bodi mpya ya Shirika la Posta Tanzania (TPC), Kanali Mstaafu, Dkt. Haruni Kondo akitoa neno la shukrani mbele ya Waziri Mhandisi Isack Kamwelwe.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (katikati), katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi hiyo na Postamasta Mkuu, Hassan Mwang’ombe (kulia) na mwakilishi wa Katibu Mkuu wizara hiyo (Sekta ya Mawasiliano), Kitolina Kippa (wa pili kulia).
Picha ya pamoja ya Waziri Mhandisi Isack Kamwelwe na wajumbe wa bodi pamoja na Menejimenti ya Shirika, mara baada ya kumaliza uzinduzi huo katika ukumbi wa mikutano uliopo katika Jengo la Makao Makuu ya Bandari.