Home Mchanganyiko WAISHI MTINI SIKU TANO BILA KULA CHAKULA KUKWEPA MAFURIKO

WAISHI MTINI SIKU TANO BILA KULA CHAKULA KUKWEPA MAFURIKO

0

Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Hashim Mgandilwa akiambatana na kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Ruangwa Leo tarehe 28/01/2020 ameshiriki katika tukio la kuokoa watu walioishi katika miti kwa siku tano bila ya kupata chakula.

Watu watatu kutoka familia moja wameishi juu ya mti tangu tarehe 24/1/2020 ambapo mvua kubwa ilianza kunyesha iliopelekea kufurika kwa maji kutokea mto mbwemkuru

Akizungumza Mara baada ya kuwaokoa watu hao mkuu wa wilaya ya Ruangwa amewashukuru wananchi kwa kuendelea kujitoa katika kuwatafuta watu hao hadi kuwapata wakiwa juu ya miti,huku wakiwa hai.

Mkuu wa wilaya amesema huu ni mfano wa kuigwa na jamii kwa kuwa na umoja wakati wa matatizo.

Mwisho mkuu wa wilaya ya Ruangwa ameendelea kuwaomba wananchi wa wilaya ya Ruangwa kuendelea kuchukua tahadhari na waangalifu katika kipindi hiki cha mvua kubwa zinazoendelea kunyesha