Home Michezo SAMATTA ACHEZA DAKIKA 65,ASTON VILLA YATINGA FAINALI CARABAO,YAICHAPA 2-1 LEICESTER CITY

SAMATTA ACHEZA DAKIKA 65,ASTON VILLA YATINGA FAINALI CARABAO,YAICHAPA 2-1 LEICESTER CITY

0

MBWANA Samatta, mshambuliaji wa timu ya Aston Villa, amecheza mchezo wake wa kwanza usiku wa wa kuamkia leo mbele ya Leicester City kwenye Kombe la Carabao, Uwanja wa Villa Park na timu yake imetinga hatua ya fainali.

Aston Villa ililazimisha ushindi kibabe wa  mabao 2-1 na bao la Aston Villa la kuongoza lilifungwa na Matt Target dakika ya 12 kwa shuti kali lililomshinda mlinda mlango wa Leicester City na Leicester walisawazisha bao hilo dakika ya 72 kupitia kwa Kelechi Iheniacho.

Bao pekee la ushindi la Aston Villa lilifungwa dakika ya 90+3 na Mohamoud Hassan.

Samatta alifunga bao la kwanza kwenye mchezo wake wa leo dakika ya 37 ila mshika kibendera alidai kuwa mtoa pasi alikuwa ameotea.

Dakika ya 64 Samatta alikosa bao la wazi akiwa na mlinda mlango kwa kushindwa kuitumia pasi ya mchezaji mwenzake akiwa ndani ya 18 jambo lililomuuza nyota huyo

Dakika ya 66 Samatta alitolewa nje na nafasi yake ilichukuliwa na Keinan huku Wachezaji wawili wa Aston Villa walionyeshwa kadi ya njano ambao ni Konsa na Luiz.

Aston Villa wametinga Fainali ya michuano hiyo huku wakimsubiri mshindi kati ya Manchester City au Man United na wameitoa Leicester City kwa jumla ya mabao 3-2.