Home Mchanganyiko KIVUKO CHA MV. ILEMELA CHAFANYIWA MAJARIBIO

KIVUKO CHA MV. ILEMELA CHAFANYIWA MAJARIBIO

0

Mbunge wa Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angelina Mabula katikati akiwapungia mkono wakazi wa Kayenze (hawapo pichani) wakati akishuka kutoka kwenye kivuko cha MV. Ilemela mara baada ya kuwasili eneo la Kayenze wakati kikifanyiwa majaribio. Kivuko hicho kimejengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 2.7 na kina na uwezo wa kubeba abiria 200 na magari 10 sawa na tani 100.

Mamia ya wakazi wa maeneo ya Kayenze wanaonekana wakiwa mbele ya kivuko hicho wakisikiliza hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa katika tukio la majaribio ya kivuko cha MV. Ilemela lililofanyika katika eneo la Kayenze.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle akizungumza na wananchi wa Kayenze ambapo alitoa taarifa fupi ya ujenzi wa kivuko hicho wakati wa tukio la majaribio ya kivuko cha MV. Ilemela lililofanyika katika eneo la Kayenze. Kushoto ni Mbunge wa Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Mendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angelina Mabula.

Mbunge wa Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angelina Mabula akizungumza na wakazi wa Kayenze (hawapo pichani) wakati wa tukio la majaribio ya kivuko cha MV. Ilemela lililofanyika katika eneo la Kayenze.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza Dkt. Anthony Diallo (mbele) akishuka kutoka kwenye kivuko cha MV. Ilemela mara baada ya kukikagua  kivuko hicho katika eneo la yadi ya Songoro wakati kikisubiri kuanza kufanyiwa majaribio. Kivuko cha MV. Ilemela kimejengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 2.7 na kina na uwezo wa kubeba abiria 200 na magari 10 sawa na tani 100.

Baadhi ya wakazi wa maeneo ya Kayenze wakiwa ndani ya kivuko cha MV. Ilemela wakati wa tukio la kukifanyia majaribio. Kivuko hicho kinatarajiwa kuanza kutoa huduma hivi karibuni kati ya maeneo ya Kayenze na visiwa vya Bezi. MV. Ilemela imejengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 2.7 na ina na uwezo wa kubeba abiria 200 na magari 10 sawa na tani 100.

PICHA ZOTE NA TEMESA (MWANZA)