Home Mchanganyiko TanTrade Yatoa Semina Kwa Wabunge wa Kamati ya Bunge ya Viwanda,Biashara na...

TanTrade Yatoa Semina Kwa Wabunge wa Kamati ya Bunge ya Viwanda,Biashara na Mazingira

0

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya  Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Edwin Rutegaruka,akitoa semina kwa wabunge wa Kamati ya Bunge ya viwanda, Biashara na Mazingira iliyoandaliwa na Mamlaka ya  Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bungeni jijini Dodoma

Sehemu ya wabunge wa Kamati ya Bunge ya viwanda, Biashara na Mazingira,wakifatilia semina inayotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya  Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Edwin Rutegaruka,iliyoandaliwa na Mamlaka ya  Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bungeni jijini Dodoma

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Bw.Ludovick Nduhiye, akieleza majukumu ya TanTrade  katika semina ya wabunge wa Kamati ya Bunge ya viwanda, Biashara na Mazingira iliyoandaliwa na Mamlaka ya  Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Bungeni jijini Dodoma

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda,Biashara na Mazingira Mhe.Kanali Mstaafu,Masoud Ali Khamis akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ushauri wa kamati hiyo kwa Mamlaka ya  Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade).

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya  Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) Edwin Rutegaruka,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kuwapa semina wabunge wa Kamati ya Bunge ya viwanda, Biashara na Mazingira bungeni jijini Dodoma

…………….

Na.Alex Sonna,Dodoma

Serikali imeshauriwa kuona namna ya kuongeza  kodi kwa bidhaa zinazotoka Nje ya Nchi ili ziende sawa na zile zinazozalishwa hapa nchini lengo ni kulinda bidhaa zinazozalishwa hapa nchini nazo kupata soko.

Ushauri huo umetolewa  Jijini Dodoma na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Viwanda Biashara na Mazingira, Kanali Mstaafu,Masoud Ali Khamis wakati akizungumza katika semina iliyoandaliwa na  Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRAD).

Khamis ambaye ni Mbunge wa Mfenesini (CCM) amedai kwamba viwanda vya ndani vimekuwa vikikabiliwa na changamoto ya bei katika soko kuwa kubwa kuliko bidhaa zinazotoka nje ya Nchi hivyo ameishauri Serikali  kuangalia namna ya kuongeza kodi kwa bidhaa zinazotoka Nje ya Nchi ili ziendane na bidhaa za ndani. 

“Lakini itafutwe mbinu ya kufanywa hapa ili wenzetu wa viwanda vya ndani wauze bidhaa zao tatizo letu kubwa la viwanda vya Tanzania ni bidhaa zetu kuwa zina bei ya juu na ‘Production Cost’ ya viwanda vyetu ipo juu kuna umeme na mambo mengine mengi,” amesema Khamis.

Ameongeza kuwa “Kwa sababu wangetumia matumizi ya chini sasa hivi kiwanda kinaweza kuzalisha mali zikajaa kwenye magodauni wafanyakazi bado anao hawafanyi kazi lakini anawalipa mishahara na hili ni tatizo”amesema.

Kuhusu changamoto ya baadhi ya viwanda kukosa masoko,Makamu Mwenyekiti huyo amesema jambo hilo sio mara ya kwanza kulifikisha Serikalini ambapo amesema kwamba linahitaji kuangaliwa kwa umakini.

Kwa upande wake,Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya  Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE)Edwin Rutegaruka amesema wameweka mikakati  endelevu ya kuzalisha bidhaa kulingana na mahitaji ya soko.

Pia,amebainisha kuwa wameangalia namna gani ya kuwaunganisha wazalishaji ili  waweze kuzalisha bidhaa zinazohitajika sokoni kwa kuanzisha vikundi ambavyo vitawapa majibu kujua mahitaji ni yapi katika soko ili waweze kufanya biashara zao kwa urahisi.

“Pia tuna Intelejensia ya masoko, tumeweka mpango mkakati wa kuyaelewa masoko yanataka nini tunatarajia 2020 tuweke mifumo mizuri na kwa kuanzia tayari tuna Maafisa Masoko 35 kwa ajili ya kujua soko linataka nini na tutaanza na masoko  ya jirani yanataka nini na baadae tutaenda katika masoko makubwa yanataka nini” amesema.