Home Mchanganyiko KERO ZA WANUNUZI ZATAJWA KURUDISHA NYUMA ZAO LA TUMBAKU

KERO ZA WANUNUZI ZATAJWA KURUDISHA NYUMA ZAO LA TUMBAKU

0

Kero za  wanunuzi wa zao la tumbaku  zimetajwa kama chanzo cha kurudisha nyuma zao  na kuongeza changamoto katika biashara hiyo. 

Akiongea wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya  Bodi ya Tumbaku katika kikao kilichofanyika hivi karibuni kwenye ukumbi wa mikutano wa Wizara ya Kilimo, Kaimu Mkurungenzi Mkuu wa Bodi ya Tumbaku Bwana Stanley Mnozya  amesema kero hizo zinasababishwa na kesi baina ya wanunuzi wa tumbaku na Tume ya ushindani.

Amesema makampuni matatu (3) kwa pamoja yanadaiwa kiasi cha shilingi Trilion 7 kiasi ambacho kinatokana na tume ya ushindani kubaini kuwa kampuni hizo hazikuonesha ushindani katika biashara ambapo kiasi hicho kimekuwa kikubwa sana .

Aidha Bwana Mnozya   amesema kuchelewa urejeshwaji wa kodi ya ongezeko la thamani  VAT ambapo kampuni hizo zinaidai serikali tangu mwaka 2016 takribani 42.4 bilioni. Aliishukuru Serikali kwa kuendelea kulifanyia kazi suala hii na hasa ahadi ya Mhe. Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli wakati akizungumza na Mabalozi wa Nchi Mbalimbali kuwa marejesho hayo yatafanyika baada ya uhakiki

“Sambamba na kurekebishwa kasoro na kesi za  mapato kupitia Transifer pricing ambapo baadhi ya makampuni yametakiwa kulipa faini kubwa” . alisema Bwana Mnozya.

Hata hivyo bwana Mnozya ameiomba serikali  kutatua changamoto hizo kwa wakati ili kuondoa changamoto hizo ambazo zimekuwa zikiikabili na kuithiri sekta ya tumbaku kwa kipindi kirefu sasa.

Amesema kama hataua za utatuzi hazitachukuliwa kuna hatari ya wanunuzi kushindwa kuendesha biashara ya tumbaku kulingana na kiasi cha madeni wanachotakiwa kulipa kuwa kikubwa. Aidha zitarudisha nyuma jitihada za Bodi za kutaka kuongeza kilimo cha tumbaku kufikia tani 150,000 ifikapo 2024/2025

Bwana Mnozya pia, amemuomba Waziri wa Kilimo Mhe. Japhet Hasunga  kukutana na Waziri wa Viwanda na Biashara ili kujadiliana namna ya kupata masoko ya nchi za COMESA zikihusisha  Misri, Algeria na Sudani kutokana na uhitaji mkubwa wa tumbaku katika nchi hizo.

“Nchi za COMESA wanahitaji tumbaku ya Tanzania lakini  hatuna uanachama na nchi hizo” alisema Mnozya.

Awali amebainisha kwamba kufikia Desemba 15/2019 tani 70,087 zenye thamani ya fedha za kitanzania 230,367,663,073 zimenunuliwa na kuvuka lengo la kununua tani 55,000 huku ajira ikiongezaka na kufikia 1,400,000.