Baadhi ya Wanachama wa Jumuiya isio ya Kiserikali ya FAWE waliohudhuria katika Mkutano Mkuu wa Tisa uliofanyika katika Ukumbi wa Skuli ya Hailesselasie Mjini Unguja.

Mke wa Rais Mstaafu  wa Awamu ya Tano Mama Shadya Karume akikata Keki kusherehekea kutimia miaka 20  ya Jumuiya ya FAWE katika Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Tisa wa Jumuiya Uliofanyika katika Ukumbi wa Skuli ya Hailesselasia Mjini Unguja.

Mratibu wa Fawe Zanzibar Hinda Abdalla Ajmiy akitoa taarifa ya FAWE katika Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Tisa wa Jumuiya Uliofanyika katika Ukumbi wa Skuli ya Hailesselasia Mjini Unguja.

Mmoja kati ya Wanafunzi waliopata Msaada  kutoka Jumuiya ya Fawe ambae amesomea Apphed Chemistry Nchini China Thania Salum Nassor akitoa maelezo katika Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Tisa wa Jumuiya Uliofanyika katika Ukumbi wa Skuli ya Hailesselasia Mjini Unguja. 

Mwenyekiti wa FAWE Zanzibar Dk,Mwatima Abdalla akitoa hotuba ya makaribisho kwa mgeni Rasmi  katika Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Tisa wa Jumuiya Uliofanyika katika Ukumbi wa Skuli ya Hailesselasia Mjini Unguja. 

Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tano Mama Shadya Karume akisisitiza jambo wakati akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Tisa wa Jumuiya ya FAWE Uliofanyika katika Ukumbi wa Skuli ya Hailesselasia Mjini Unguja. 

Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tano Mama Shadya Karume  akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Tisa wa Jumuiya ya FAWE Uliofanyika katika Ukumbi wa Skuli ya Hailesselasia Mjini Unguja. 
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

…………….

Na Rahma Khamis Maelezo          

Mlezi wa Mtandao wa kuwasaidia watoto wa kike kupata maendeleo ya Elimu (FAWE)  Zanzibar Mama Shadia Karume amezitaka Jumuiya zisizo za kiserekali kuwasaidia watoto wa kike  wanaoishi katika mazingira magumu ili kufikia malengo waliojiwekea.

 Ameyasema hayo alipokuwa akifungua Mkutano mkuu wa tisa wa Jumuiy ya FAWE  katika Ukumbi wa a Skuli ya Sekondari ya Haileselassie.

 Amesema kumpatia elimu mtoto wa kike ni msingi mzuri katika kulinda familia hivyo ni muhimu taasisi za kiraia kushirikiana na Serikali kuwapatia  elimu hasa masomo ya Sayansi na Teknolojia ili waweza kujitegemea  na kujikwamua katika  hali ngumu yamaisha.

Aidha amsema kuwa program ya Tuseme ni muhimu sana kwa  wanawake  kwani inawafanya watoto wa kike  kujiamini na kuwasaidia katika kujieleza kuwa yeye ni nani na anataka nini .

Mama Shadia ameongeza kuwa masomo ya Sayansi yanawasaidia vijana kiuchumi na kijamii hivyo ameipongeza Jumuiya ya FAWE kwa kuanzisha program ya Stemp kwa wanaume na wanawake.

Mama Shadya amezishauri Taasisi za Kiraia kuisaidia Jumuiya hiyo na kuwataka vijana kujiunga na FAWE ili waweze kunufaika  na elimu inayotolewa.

Mratibu wa Jumuiya ya FAWE Hinda Abdallah Ajmy mesema kuwa wameamua kuwashirikisha watoto wa kie wengi zaidi kuliko wanaume kutokana na woga walionao na itahakikisha inawasaidia kuwajengea uwezo wa kujiamini.

Amesema wamekuwa wakitoa ushauri kwa Wizara  ya Elimu ili kuhakikisha kuwa mtoto wa kike anasaidiwa kupata elimu hata wale ambao uwezo wao wa kusoma ni mdogo kutokana na mazingira yasiyorafiki ya maisha.

Aidha amefahamisha kuwa wameanzisha mradi wa fadhili watoto mayatima   na kuwasaidia watoto zaidi ya 200 wanaishi katika mazingira magumu wanume na wanawake Unguja na Pemba.

Mwenekiti wa Jumuiya hiyo Dkt, Mwatima Abdallah amewaomba viongozi waliochaguliwa kuendelea kuwa na moyo wa kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu ili na wao wapate elimu.

Akitoa ushuhuda, mwanafunzi Amina Omar Kitwana kutoka Klabu ya Tuseme amesema kuwa mafunzo aliyopatiwa yamemsaidia kuwa na uwelewa kuweza kujiamini popote.

Sambamba na hayo wanafunzi ambao wamefadhiliwa kimasomo na FAWE wameahidi kuyafanyia kazi waliyoyaahidi wakati walipotaka ufadhili huo

Fawe imenziswa mwaka 1998 na ina wanachama 140 kutoka Unguja na Pemba ambapo Kauli mbiu ni FAWE ZANZIBAR KUWA KARIBU NA WASHIRIKI WA MAENDELEO KUMUENDELEZA MTOTO WA KIKE KIELIMU