Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza akizungumza na wadau wa tasnia ya filamu Mkoa wa Singida leo na kuwasisitiza
kurasimisha kazi zao pamoja na kujisajili,katika kikao cha kusikiliza kero za wadau hao na kuwaeleza mikakati ya serikali katika kuimarisha tasnia hiyo kilichoandaliwa
na Bodi ya Filamu Tanzania.
Kaimu Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Dkt.Kiagho Kilonzo akizungumza na wadau wa tasnia ya Filamu Mkoa wa Singida leo kuhusu mikakati ya bodi ya filamu
katika kuimarisha mazingira ya usambazaji wa kazi za filamu nje ya nchi ambapo wameipata kampuni kutoka Nigerea itakayo nunua filamu mia moja zenye hadithi za
asili ya kitanzania,wapili kushoto ni Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza ,wa kwanza kushoto ni Katibu Tawala Wilaya ya
Singida Wilson Shimo na wa kwanza kuliani Afisa Utamaduni Mkoa wa Sngida Bw.Hendry Kapera.
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza aliyeketi watatu kushoto akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa tasnia ya filamu Mkoani Singida leo mara baaada ya kulamizika kikao cha kusikiliza kero za wadau hao na kueleza mipango ya serikali katika kuimarisha sekta hiyo na kuthibibiti uharamia wa kazi za filamu na kuhakikisha msanii ananufaika na kazi yake,wa pili kulia Kaimu ni
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Dkt.Kiagho Kilonzo pamoja na Katibu Tawala
Wilaya ya Singida Wilson Shimo.
Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza (aliyeketi watatu kushoto) akitizama filamu ya masanii wa filamu Maria Luya
aliyomkabidhi wakati alipokuwa akifanya kikao na wadau wa tansia ya filamu mkoa wa singida hawapo pichani,wa kwanza kulia ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu
Tanzania Dkt.Kiagho Kilonzo, na wapili kushoto ni Katibu Tawala Wilaya ya Singida Wilson Shimo.
***************************
Na Anitha Jonas – WHUSM
22/01/2020
Singida.
Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Juliana Shonza
amewasisitiza wanatasnia ya filamu kuhakikisha wanarasimisha kazi zao na kujisajili.
Mheshimiwa Shonza ametoa agizo hiyo leo Mkoani Singida alipokuwa akifanya kikao na wadau wa tasnia ya filamu wa mkoa huo kwa lengo la kutaka kusikiliza kero zao na
kuwaeleza wadau hao mikakati ya serikali katika kuboresha tasnia hiyo,kuthibiti
uharamia ili kuhakikisha wanafaidika na kazi zao.
Akiendelea kuzungumza katika kikao hicho Naibu Waziri huyo aliwasisitiza wanatasnia hao wa filamu kuzingatia suala la uandaaji wa muswada wa filamu na kupeleka
miswada hiyo kwa maafisa utamaduni kwa ajili ya ukaguzi na kupata ushauri wa filamu watakayoandaa sababu hiyo ni moja ya njia itakayosaidia kuandaa kazi zenye
ubora.
“Kwanza ningependa niwashauri muache kusambaza au kuuza kazi zenu kwa njia ya ‘flash’ katika vibanda vya kuuza filamu sababu hii bado ni njia inayowakandamiza na
hauwezi kupata faida ya kazi yako, sasa hivi kazi hizo za filamu zinasambazwa kwa mfumo wa kidigitali mfano kwenye Swahilifilx na Netflix,kikubwa ni kazi yako iwe
yenye ubora na iliyozingatia utaratibu wa kitaalamu katika kuandaa filamu ikiwemo wachezaji kuvaa uhusika na kucheza katika maeneo yenye uhalisia wa filamu
hiyo,”alisema Mhe.Shonza.
Naye Kaimu Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Dkt.Kiagho Kilonzo bodi imekuwa ikitoa mafunzo kwa wadau wa tasnia hiyo kwa lengo la kuwajengea uwezo
wa kuandaa kazi bora zitakazo kuwa na ushindani kwa ndani na nje ya nchi na kwa hivi karibuni wanatarajia kufanya mafunzo hayo mkoani Dodoma na kwa wadau wa
Singida ambao hawajawahi kupata mafunzo hayo wanakaribishwa kushiriki.
“Bodi ya filamu katika kuimarisha masoko ya usambazaji wa filamu ndani na nje ya nchi imempata mdau kutoka Nigeria mwenye Kampuni iitwayo ENVIVO ambaye yupo
tayari kununua jumla kazi mia moja mpaka ifikapo mwezi Juni mwaka huu,zenye hadithi mbalimbali za kitanzania ambapo zitatafsiriwa kwa lugha kwa lugha ya
Yoruba,Pijini na Igbo kusambazwa,kikubwa katika kazi hizo ni ziwe zimebeba hadithi za kitanzania na zenye ubora na pia ziwezinaendana na muswada,”alisema
Dkt.Kilonzo.
Pamoja na hayo Dkt.Kilonzo aliwasihii wadau hao kuwa mfumo wa usambazajiwa kwa kazi za filamu kwa sasa umebadilika na filamu kwa sasa mara baada ya kukamilika
inafanyiwa uzinduzi katika majumba ya sinema na huko itaonyeshwa kwa kipindi fulani na baadae inapelekwa katika mifumo mingine ya kidigitali na hatua ya kuiweka
katika CD na Youtube niyamwisho hii ni katika kulinda kazi hizo na uharamia pia kuhakikisha msanii anapata faida ya kazi yake.
Kwa upande wa Afisa Utamaduni Mkoa Bw.Hendry Kapera alisema wasanii wengi wa filamu katika mkoa huo hawataki kujisajili wala kurasimisha kazi zao hii ni
changamoto kubwa na wamekuwa wakijiweka mbali na maafisa utamaduni wa wakihofia kuulizwa kuhusu usajili na hii imechangia wao kuandaa kazi zisizo na ubora
sababu hawapendi kushirikiana na maafisa hao.
Halikadhilika nae mmoja ya wasanii hao wa filamu kutoka Wilaya ya Ikungi Bw.Salumu Ntandu aliomba bodi ya filamu kuwapatia mafunzo wadau hao wa mkoa
huo na pia aliwasihii wasanii wenzake kuwa na umoja na kuacha migogoro kwani umoja wao ndiyo utakaoweza kutangaza kazi zao na kutangaza mkoa wao pale
watakapo andaa kazi nzuri zenye ubora na kushirikishana katika kuitangaza na kuizindua.