Home Uncategorized IGP SIRRO TUTAENDELEA KUCHUKUA HATU KALI ZA KISHERIA

IGP SIRRO TUTAENDELEA KUCHUKUA HATU KALI ZA KISHERIA

0

******************************

23/01/2020 KAHAMA, SHINYANGA

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro ameendelea kuwaonywa wananchi kuacha kujihusisha na vitendo vya mauaji yanayotokana na imani za ushirikina na kwamba amesisitiza kuwa, suala la amani ni la umuhimu hususani
kwa maendeleo ya taifa.

 

IGP Sirro amesema hayo akiwa Kakola Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga, ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya kikazi mkoani humo ambapo ameitaka jamii kushirikina na vyombo vya dola katika
kuhakikisha suala la amani linaendelea kudumishwa nchini.

 

Akizungumza kwa niaba ya wananchi wa Kakola Kilikili James amesema kuwa, wapo watu wanaofahamika ambao wamekuwa wakijihusisha na ramli chonganishi na hivyo wapo tayari kutoa ushirikiano kwa vyombo vinavyohuzika
ili wachukuliwe hatua kali za kisheria.