Home Mchanganyiko TUMIENI FURSA ZA UJIO WA UMEME KUBADILISHA MAISHA: MBUNGE WA CHALINZE RIDHIWANI...

TUMIENI FURSA ZA UJIO WA UMEME KUBADILISHA MAISHA: MBUNGE WA CHALINZE RIDHIWANI KIKWETE

0
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
MBUNGE
wa Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete amewataka wakazi wa kijiji cha Talawanda
kutumia fursa za ujio wa nishati ya umeme kubadilisha maisha yao.
Mheshimiwa
Kikwete ameyasema hayo wakati akihutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika
kwenye viwanja vya zahanati ya kijiji hicho ambapo Naibu Waziri wa Nishati Mhe.
Subira Mgalu alifika kukagua maendeleo ya upelekaji wa mradi wa umeme kwenye
kijiji hicho chini ya mpango wa REA awamu ya tatu mzunguko wa kwanza kwa wigo
wa nyongeza (ADDENDUM).
“Ndugu
zangu tutumie vizuri rasilimali hii inayokuja, ukienda pale Chalinze miaka 25
iliyopita haikuwa Chalinze unayoiona leo, lakini leo ukienda pale mambo
yamebadilika, watu wanaweza kufanya kazi mchana wakatijua linawaka na usiku jua
linapopotea kwa sababu ya nishati ya umeme.” Alisema Mhe. Kikwete na kuongeza…………………….  Lakini pia hata vyakula mtunavyokula sasa,
zamani tulikata miti kwa kiwango cha juu kwa matumizi ya nyumbani, matokeo yake
tunageuza eneo letu jangwa sasa hivi inaelekea tatizo hilo kuisha kwa sababu
umeme umekuja.
Pia
amesema Serikali inaendelea na ujenzi wa mradi mkubwa wa umeme wa Julius
Nyerere kule Rufiji, mradi ukiisha kituo kikubwa cha kupoza umeme kitajengwa
Chalinze na hivyo wanakijiji wa Talawanda na wana Chalizne wote wanapaswa
kutumia fursa hizo ipasavyo.
Mbunge
huyo wa Chalinze amelipongeza Shirika la umeme nchini TANESCO na wakala wa
umeme vijijini REA kwa kasi ya upelekaji umeme kwenye maeneo ya vijiji vya
jimbo la Chalinze ambapo umeme unaenda kuleta mabadiliko makubwa ya maisha ya
wananchi.
 MBUNGE wa Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete, akihutubia kwenye mkutano huo Januari 21, 2020
 Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu, akihutubia wananchi wa kijiji cha Talawanda Januari 21, 2020 wakati w aziara yake ya kukagua maendeleo ya upelekaji wa mradi wa umeme kwenye vijiji vya Talawanda na Kibindu jimbo la Chalizne Mkoani Pwani.
 Mhe. Kikwete akijadiliana jambo na wananchi wa jimbo lake huko kijiji cha Talawanda.
 Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Subira Mgalu akimsikiliza Mbunge wa jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete wakati wa ziara hiyo.
 MBUNGE wa Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete, akihutubia kwenye mkutano huo Januari 21, 2020
 Baadhi ya wanakijiji wakisikiliza 
 Baadhi ya wanakijiji wakisikiliza